Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Sunday, 6 July 2014

Chile na Mexico hawakustahili kutolewa mapema Kombe la Dunia

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Madaraka Selamani,timu za Chile na Mexico,zili staili kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka huu kutokana na kiwango walichoonesha.
Madaraka aliyewahi kuichezea klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuibebesha ubingwa wa Tanzania bara mara tatu,alizitaka timu za Afrika kuiga mfano wa timu hizo kutokana ushindani waliouonyesha licha ya kutolewa katika hatua ya mtoano.
“Timu za Afrika zinapaswa kuiga mfano wa timu za Chile na Mexico,ambazo hazikuwa na wachezaji wenye majina makubwa lakini zilionyesha ushindani wa kweli na kuwatoa jasho waandaji wa fainali hizo Brazili,”alisema Madaraka.
Mkongwe huyo pia alisema haipi nafasi Brazili ya kunyakua ubingwa huo kwa sababu imeonyesha kuwa na mapungufu mengi licha ya kufika hatua hiyo ya robo fainali.
“Hii siyo Brazili ile ambayo tulikuwa tunaifahamu ambayo huiwezi kumaliza dakika 90, pasipo kutikisa nyavu za wapinzani tumeshuhudia mechi mbili ile ya

Thursday, 2 May 2013

BREAKING NEWS: FIFA YAWARUDISHA WAMBURA NA MALINZI

Malinzi, Wambura warudishwa kugombea TFF na FIFA.


Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
 
 
Kuna taarifa kwamba wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 

Thursday, 11 April 2013

SAKATA NA KUFUNGIWA KOCHA BILAL LACHUKUA SURA MPYA



Ikiwa ni ni takribani siku tatu tu baada ya kamati ya ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania-TFF kumfungia kocha msaidizi wa Toto African ya Mwanza Athumani Bilal mechi tatu kwa kosa la kumshambulia kwa maneno kocha mkuu wa timu ya TZ Prisons Jumanne Challe sakata hilo limechukua sura mpya.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Afya Radio 96.8mhz kocha Athumani Bilal amekana ‘kumtukana ‘ kocha Jumanne Challe wa Tz Prisons  anasema, ‘TFF nawashangaa sana sijamtukana na siwezi kabisa kumtukana mwalimu wangu aliyenifundisha kazi Jumanne Challe na pia siwezi kabisa kumtukana mtu yeyote Yule,ningekuwa nimemtukana ingewezekana vipi baada ya mechi tuwe wote!?’ Anahoji Bilal na pia mbona sijahojiwa na mtu yeyote au chombo chochote wanaishia tu kuhukumu ndo kazi zinavyofanyika hivyo?
Michezo na Afya ilipotaka kujua kilichosababisha yeye kutolewa kwenye benchi la ufundi Bilal alijibu mpaka sasa sijui na sijui hata Yule kamisaa aliandika nini kwenye ripoti yake.


Tuesday, 9 April 2013

SIR ALEX AZUNGUMZIA GEMU YA JANA

Sir Alex Ferguson amedai Manchester United walikosa ‘bahati’ kwa kufungwa 2-1 na Manchester City hapo jana na pia alikiri kuwa, Siku zote, Timu yake ‘hujibebesha zigo’ badala ya kurahisisha kazi.
Ingawa jana walifungwa, Man United bado wapo kileleni wakiwa Pointi 12 mbele ya Man City na Mechi zikiwa zimebaki 7.
Kwa hali ilivyo sasa, Man United wanahitaji kushinda Mechi 3 na Sare 1 kati ya hizo Mechi zao 7 ili watwae Ubingwa ikiwa Man City watashinda Mechi za mbele yao.












TFF YATOA ADHABU KWA KLABU NA MAKOCHA VPL

TFF_LOGO12
KLABU ya Yanga na Kocha Msaidizi wa timu ya Toto Africans, Athuman Bilali wamepigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja kutokana na makosa mbalimbali katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea nchini.
Adhabu hizo zimetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili (Aprili 7 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za waamuzi na makamishna kwa michezo namba 108 hadi 171.

KAMATI YA TFF YAZIPONGEZA ASHANTI, MBEYA CITY, RHINO

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/20114).
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu.

PATASHIKA YA KUJINASUA KUSHUKA DARAJA KESHO

Polisi Morogoro inapambana na Ruvu Shooting katika moja kati ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa kesho (Aprili 10 mwaka huu). Matokeo ya mechi hiyo yanatarajia kutoa mwanga kama Polisi inaweza kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.
Timu hiyo itakuwa nyumbani Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mechi hiyo itakayochezeshwa na Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga akisaidiwa na Godfrey Kihwili na Ephrony Ndissa wa Arusha.
Polisi Morogoro inayonolewa na Adolf Rishard inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na pointi 18 tu na imebakiza mechi tatu dhidi ya Simba, Kagera Sugar na Coastal Union.
Mechi nyingine za kesho ni kati ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 20 dhidi ya Mgambo Shooting. Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mgambo ina pointi 24 na iko katika nafasi ya tisa.
Mwamuzi Said Ndege wa Dar es Salaam atachezesha mechi kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Toto Africans itakayofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Toto Africans ya Kocha John Tegete ina pointi 21 ikiwa nafasi ya 11 wakati Mtibwa Sugar iko nafasi ya tano na pointi zake 32.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 11 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Azam na African Lyon itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex.

Monday, 8 April 2013

TAKUKURU yawasafisha wachezaji Azam

TAKUKURU YAWASAFISHA WACHEZAJI WA AZAM
AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

S. L.P. 42325,
Temeke,
Simu: 022 2850633,
Nukushi: (022) 2850635,
Baruapepe:rbctemeke@pccb.go.tz,
Mtandao www.pccb.go.tz

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UCHUNGUZI WA WACHEZAJI WA TFF
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa taarifa kwa umma kwamba, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Temeke dhidi ya wachezaji wanne wa timu ya soka ya AZAM waliokuwa wakituhumiwa kupokea hongo/rushwa ili kupanga matokeo, haukuweza kuthibitisha tuhuma hiyo.

Takwimu mbalimbali kuelekea mechi ya leo kati ya Man Utd vs Man City

Kama una wasiwasi na Saa yako, Fanya kurekebisha Tym Mapemaaa... Tukutane Saa Nne Usiku pale The Vibe Leo.!! #Powered by The Vibe Club-Mbeya#
TAKWIMU MBALIMBALI KUELEKEA MECHI YA LEO YA WATANI WA JADI KUTOKA JIJI LA MANCHESTER-'MANCHESTER DERBY'
Mchezo wa usiku wa leo utakuwa ni wa 165
kukutana.

Ushindi:
Man Utd 69.
Man City 45.
Sare 50.