Ikiwa ni ni takribani siku tatu tu baada ya kamati ya ligi
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania-TFF kumfungia kocha msaidizi wa Toto
African ya Mwanza Athumani Bilal mechi tatu kwa kosa la kumshambulia kwa maneno
kocha mkuu wa timu ya TZ Prisons Jumanne Challe sakata hilo limechukua sura
mpya.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Afya Radio 96.8mhz
kocha Athumani Bilal amekana ‘kumtukana ‘ kocha Jumanne Challe wa Tz Prisons anasema, ‘TFF nawashangaa sana sijamtukana na
siwezi kabisa kumtukana mwalimu wangu aliyenifundisha kazi Jumanne Challe na
pia siwezi kabisa kumtukana mtu yeyote Yule,ningekuwa nimemtukana ingewezekana
vipi baada ya mechi tuwe wote!?’ Anahoji Bilal na pia mbona sijahojiwa na mtu
yeyote au chombo chochote wanaishia tu kuhukumu ndo kazi zinavyofanyika hivyo?
Michezo na Afya ilipotaka kujua kilichosababisha yeye
kutolewa kwenye benchi la ufundi Bilal alijibu mpaka sasa sijui na sijui hata Yule
kamisaa aliandika nini kwenye ripoti yake.
Michezo na Afya haikuishia hapo iliamua kumtafuta kocha
Jumanne Challe:-
Mtangazaji: Hallow kocha,unaongea na Michezo na Afya Radio
kutoka MWZ TZ, habari ya kazi?
Challe: Safi Mungu anasaidia kazi inaenda vizuri na
tunaendelea kuhakikisha timu yetu haishuki daraja.
Mtangazaji: ok vizuri,kocha ni kwanini kocha Bilal
alikutukana?
Challe: Bilal anitukane mimi! (kwa mshangao)
Mtangazaji: Bilal kafungiwa na TFF kwasababu alikutukana
siku mlipocheza na Toto Mwanza.
Challe: sijawahi kutukanwa na Bilal na kwa nini anitukane,sasa
kama alinitukana mbona baada ya mchezo tulikuwa wote kwa muda mrefu sana
tukipiga stori mbalimbali (kwa sauti ya kuhoji na mshangao).
Mtangazaji: Asante kwa ushirikiano wako
Challe: asante na wewe na kazi njema.
Kocha Athumani Bilal amesema anakusudia kukata rufaa kwenye
kamati ya rufaa ya TFF na pia anataka aombwe msamaha sababu suala hilo anasema
limemshushia hadhi yake kwenye jamii.
0 comments:
Post a Comment