Sunday, 27 October 2013

ORODHA YA DISS TRACKS ZA KIBONGO....part one (1)


A diss track or diss song is a song primarily intended to disparage or insult another person or group. While musical parodies and attacks have always existed, the trend became increasingly common in the hip hop genre as part of the hip hop rivalry phenomenon



Ninakuletea orodha ya DISS TRACKS za kibongo kuanzia mwaka 1999/2000 to date. Katika diss tracks hizo zipo tracks ambazo msanii fulani ana mdiss msanii mwingine katika wimbo mzima ama katika baadhi ya mistari iliyomo katika wimbo huo. Na inaweza kuwa diss ya moja kwa moja au subliminal. Inaweza kuwa diss kwa msanii wa muziki, msanii wa maigizo , kiongozi au mtu yoyote maarufu.

1. MTULIZE : MABAGA FRESH DISSING INSPECTOR HAROUN & GANGWE MOBB.
Kwanza nianze kwa kuelezea chanzo cha beef kati ya Mabaga Fresh na Inspector Haroun.
Sometimes in 1999 Mabaga Fresh waliandaa show katika ukumbi mmoja wa burudani uliopo Temeke. Waliwaalika Gangwe Mobb kipindi hicho wanawika na ngoma kadhaa kama Ngangari, Mauzauza na MtuBee. Makubaliano yalikuwa malipo yatategemea na idadi ya watu watakao ingia kwenye show. Show ilitema, mtu kibao zilihudhuria show, ila kwenye malipo, Mabaga Fresh wakawaambia Gangwe Mobb , wamepata hasara, hela yote iliyo ingia wamelipia ukumbi na mambo mengine, so wakawatoa jamaa shilingi Mia Tano ( Jero). Gangwe Mobb walimind sana na hawakuwa na uwezo wa kuwapiga jamaa kwa sababu jamaa ni walemavu and all that. Kuanzia siku hiyo Mabaga Fresh wakawa Paka na Chui na Gangwe Mobb ingawa wote walikuwa kwenye koo la WALUMENDAGO.

Katika wimbo Mtulize ambao Mabaga Fresh waliurekodi kwa mara ya mwisho( walishaurekodi zaidi ya mara mbili ) mwaka 2000 kuna mistari inasema :

J.B ( Yule mwenye sauti nyembamba ) anasema “ MBELE YA CHOMBO CHA DOLA HAKUNA CHA NGANGARI”…………Hapa ana diss wimbo Ngangari wa Gangwe Mobb.



Mstari mwingine, DJ SNOXX ( Yule mwenye sauti nene ), anasema

NGEDERE NIAZIME SURA YAKO NIMTISHIE MWANANGU”
Hapa DJ SNOXX ana mock muonekano wa sura ya Inspector Haroun kwa kumfananisha na ngedere.

2. NIPO GADO ORIGINAL ( INSPECTOR HAROUN DISSING JB WA MABAGA FRESH VIA ZAY B ).
Katika wimbo huu, kuna mstari Zay B anasema “ KUBWA ZIMA KIKOJOZI, UKIULIZWA OOH NIMEPITIWA NA NJOZI “

Kwenye wimbo MTULIZE ( ambao waliurekodi kwa mara ya kwanza ), kuna mstari JB anasema “ MI SIO KIKOJOZI, ILA TU NILIPITWA NA NJOZI “
So hapa Inspector Haroun alikuwa ana mdiss JB kwa kumtumia Zay B kwenye wimbo huu.
Vile vile katika wimbo huu kuna mistari Inspector anasema “ MI NDO NYANI ,WA MWITUNI, PORINI, STERING………….” Hapa Inspector alikuwa anamjibu DJ SNOXX kwa kumwambia kuwa yeye NI NYANI akiwa na lengo la kumuonyesha kuwa hata tatizo na yeye kuitwa Ngedere.


3. NIPO GADO REMIX …………ZAY B & JUMA NATURE DISSING INSPECTOR HAROUN.
Sehemu kubwa ya wimbo huu, anasikika msanii Zay B akimdiss Inspector, baadhi ya mistari maarufu ambayo Zay B anamdiss Babu katika wimbo huu ni pamoja na
i. “ DOMO KA CHAI JABA” …Hapa Zay B ana mock muonekano wa Inspector Haroun.
ii. “ KILA UKIPITA SEHEMU ZA WATU KUJICHEKELESHA”…..Hapa Zay B ana mock tabia ya Inspekta kupenda kucheka cheka.
iii. “ WATU HAWACHOKI WAMENUNA, WAMECHOSHWA NA UREMBO WA SANAA, UNAAAMBUKIZA KINYAA “….Hapa Zay B anaponda style ya kurap ya Inspekta.
iv. ‘MI NAHISI WENZAKO WANAKUGONGA” …Hapa Zay B anamtukana Inspekta matusi ambayo wanwake huwa wanawatukana wanaume pindi wanapo kosana.



iNSPECTOR HAROUN.



Inspector Haroun akiwa na Juma Nature.




Katika wimbo huu huu kuna mstari anasikika Juma Nature akisema “ SUMBUA AKILI KIJANA USINIIGE MIMI , UTALOST , SI MTU KAWAIDA NIPO JELA NA SHIDA“…….Hili lilikuwa ni dongo kwa Inspector Haroun kuhusiana na beef lao kwamba nani kamuiga mwenzake ( Ikumbukwe kuwa Juma Nature na Inspector walikuwa wana beef la kugombea staili yao ya kuchana iliyokuwa inafanana sana huku watu wakijiuliza nani kamuiga mwenzake ).



Zay B.


4. COMPLEX ( R.I.P ) DISSING GANGWE MOBB ;
Katika wimbo wake ( Jina limenitoka ) anasikika Complex akisema “ Nimekwisha pita vyeo vyote, Uinspekta, na Uluteni now am a field marshall so u better salute me “
Kulikuwa na kutokuelewana kati ya Inspector Haroun na Complex kwa sababu Complex alikuwa anashirikiana na Zay B ambaye alikuwa na beef na Inspekta.
5. GANGWE MOBB DISSING ZAY BE & JUMA NATURE:

Katika wimbo " VIDONGE VYAO " walio mshirikisha marehemu Nasma Khamis Kidogo, Gangwe Mobb wanasikika waki wadiss wasanii na watu kibao ambao kwa mujibu wa Gangwe mobb, walikuwa wana wafanyia fitna. Wasanii walio disiwa katika wimbo huu ni pamoja na Zay B na Juma Nature.

" Kupanda chati kwa jina la Inspeector Haroun watu wana anza kuponda " mstari huu wa Inspketa unawalenga Zay B na Juma Nature. Zay B kama inavo eleweka kwa watu wengi alifahamika kwa watanzania baada ya kufanya collabo na Inspekta kwenye wimbo NIPO GADO ( Original ), na Juma Nature, kwa mujibu wa Inspekta alijulikana kwa sababu alikuwa anatumia staili ya Inspekta kurap, so Inspekta alikuwa anaamini kuwa Juma Nature amejulikana kwa sababu ya kutumia staili yake. Akifanyiwa mahojiano na gazeti moja mnamo mwaka 2001 na kuulizwa anamzungumziaje Juma Nature, Inspkta alisema anamjua Juma Nature kama msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuiga sauti yake, na ni msanii aliyefanikiwa kutangaza sanaa yake kwa kutumia jina staili ya Inspekta. Kwa ufupi huo mstari ulikuwa ni majibu kwa wimbo " Nipo Gado Remix " wa Zay B na Juma Nature.
6. JUMA NATURE DISSING INSPECTOR HAROUN KWENYE WIMBO " JINSI KIJANA "

Wimbo wa Jinsi Kijana ulitoka mnamo mwaka 2001 mwishoni, kipindi hicho beef kati ya Juma Nature na Inspekta Haroun ndo lilikuwa limepamba moto. Wasanii hawa walikuwa wanatoleana maneno ya kutambiana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama vile redio na magazeti. Wimbo wa Jinsi Kijana una muonya kijana wa kitanzania mweny tabia zilizo kinyume na maadili ya mtanzania, lakini hata hivyo ndani ya wimbo huo, kuna mistari inayo mdiss Inspekta " Vurugu zako za siri kuwa ni mtu ubinafsi,........." Hapa Juma Nature anaponda tabia ya Inspekta ya ubinafsi kwenye sanaa, ( Habari zilizokuwepo miongoni mwa wasanii wa muziki wa bongo fleva kipindi hicho ni kwamba Inspekta alikuwa mbinafsi sana kwenye gemu, alikuwa anataka asikike na kuonekana yeye tu, hata kwenye kundi lake la Gangwe Mobb, verse nyingi alikuwa anaimba yeye, rejea wimbo kama Mtoto wa Geti Kali, Luteni karama anasikika tu akiitikia " Kachumbari".

Mstari mwingine Juma Nature anasikika akisema " Na palipo na watu wengi hakosi kuwa adui, adui mfano wa nduli kakosa tabia nzuri " .

Hapa Juma Nature alikuwa anamponda Inspekta kuhusu tabia yake ya kutoelewena na wasanii wenzake wengi na ubinafsi, asilimia kubwa ya wasanii wa bongofleva walikuwa na beef na Inspekta.

Vilevile Juma NATURE anamalizia kwa kumwambia Inspekta" Najua inakuuma moyo unapo sikiliza hili song,unatamani uzime redio usisikilize mi sichongi"

COMING UP NEXT.

7. EAST COAST DISSING TMK ARTSISTS.
8. GWM DISSING EAST COAST.
9. INSPECTOR HAROUN DISSING EAST COAST.
10. WANAUME FAMILY DISSING INSPECTOR HAROUN.
11. CHEGE CHIGUNDA DISSING INSPECTOR HAROUN.
12. KIKOSI CHA MIZINGA DISSING FID Q, PROFESA JAY, BAMBOO, CHID BENZ, P.FUNK, VING’OKO, LANGA (R.I.P), BABUU, MIRAJI KIKWETE, DUDUBAYA AND TMK ARTSISTS.
13. PROFESA JAY DISSING KALAPINA.
14. MANGWEA ( R.I.P) DISSING KALAPINA.
15. CHID BENZ DISSING KALAPINA.
16. LUTENI KALAMA DISSING INSPECTPOR HAROUN.
17. INSPECTOR HAROUN DISSING LUTENI KALAMA.
18. INSPECTOR HAROUN DISSING T.M.K WANAUME.
19. JUMA NATURE RESPOND TO A INSPECTOR HAROUN DISSING LUTENI KALAMA (JUMA NATURE DISSING INSPECTOR HAROUN ON BEHALF OF LUTENI KALAMA )
20. LANGA (R.I.P ) DISSING KALAPINA & KIKOSI CHA MIZINGA.
21. PIGGY BLACK DISSING DUDU BAYA.
22. NYANDU TOZZY & CHIDY BENZ DISSING DUDUBAYA.
23. DUDUBAYA DISSING NYANDU TOZZY.
24. RADO DISSING FID Q.
25. JOH MAKINI DISSING FID Q.
26. FID Q DISSING JOH MAKINI.
27. IBRA DA HUSTLER DISSING MAPACHA.
28. NAKO 2 NAKO DISSING WATENGWA.
29. UMBWA LUTUNO WA WATENGWA ( DISSING ALL HIPHOP ARTISTS FROM DAR ES SALAAAM )
30. ROMA DISSING JOH MAKINI.
31. MANSU-LI DISSING HERMY B.
32. DULLY SYKES DISSING MWANA FA.
33. SISTER P DISSING MWANA FA.
34. WANDAGO DISSING MWANA FA.
35. INSPECTOR HAROUN DISSING MWANA FA.
36. MWANA FA DISSING INSPECTOR HAROUN.
37. PROFESA JAY DISSING FID Q.
38. SISTER P. DISSING ZAY B.
39. T.M.K WANAUME HALISI DISSING T.M.K WANAUME HALISI.
40. T.M.K HALISI DISSING T.M.K WANAUME.
41. INSPECTOR HAROUN DISSING MH. TEMBA.
42. JUMA NATURE DISSING SINTAH.
43. BWANA MISOSI DISSING SUGU.
44. SUGU DISSING MWANA FA.
45. DANI MSIMAMO DISSING MWANA FA.
46. NECK BRAKERS DISSING SOLID GROUND FAMILY.
47. DA JO DISSING ZAY B.
48. PROFESA JAY DISSING PIGGY BLACK.
49. PROFESA JAY DISSING INSPECTOR HAROUN.
50. GANGWE MOBB DISSING PROFESA JAY, SOLO THANG, MIKE TEE & OTHER ARTISTS.
51. SOLO THANG DISSING INSPECTOR HAROUN, LUTENI KALAMA, K.R. AND JUMA NATURE.
52. JUMA NATURE, K.R, AND MANGWEA (R.I.P) DISSING KALAPINA & KIKOSI CHA MIZINGA.
53. BOU NAKO & FIDOO DISSING KALAPINA.
54. FIDO & VATOLOCO DISSING KALAPINA & JOH MAKINI.
55. IBRA DA HUSTLER DISSING JOH MAKINI ( IN THE INTERVIEW ).
56. NAKO 2 NAKO & OTHER ARTISTS DISSING KIKOSI CHA MIZINGA.
57. KALAPINA DISSING WEMA SEPETU & LULU.
58. JUMA NATURE DISSING SINTAH.
59. SOLO THANG DISSING FARIDA WANJARA & WEMA SEPETU.
60. LADY JAY DEE & PROFESA JAY DISSING RUGE & KUSAGA.
61. CHID BENZ DISSING KALA PINA.
62. JAY MOE DISSING ZAHARANI.
63. SUGU DISSING INSPECTOR HAROUN.
64. BWANA MISOSI DISSING SUGU.
65. ROMA MKATOLIKI DISSING SUGU.
66. PABLO WA DAZ NUNDAZ DISSING FEROOZ WA DAZ NUNDAZ
67. DAZ NUNDAZ DISSING DAZ BABA WA DAZ NUNDAZ.
68. OTHER ARTIST , BLUE & GEEEZ MABOVU DISSING DIAMOND & OMMY DIMPOZ.
69. LORD EYEZ DISSING OMMY DIMPOZ.
70. PROFESA JAY DISSING FANANI.
NA NYINGINE NYINGI…..WAPENZI WA MUZIKI WA BONGOFLEVA/BONGO HIP HOP, ENDELEA KUFUATILIA UZI HUU

Kwa ushirikiano na JF MEMBERS kwa sapoti ya nguvu kutoka kwa LIKUD

0 comments:

Post a Comment