Kutokana
na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Judith Wambura ‘Lady JayDee’
kuonekana kutuma ‘Tweets’ zilizobeba mafumbo huku akitoa mazito ya
moyoni juu ya mtu anayemvurugia mipango yake ya kimuziki hakuweza
kumtaja jina mume wake Gadna Habash afunguka juu ya ‘Tweets’ hizo
Akizungumza jijini Dar es Salaam hili hivi karibuni Gadna alisema
kuwa ‘tweets’ alizoziweka msanii huyo zinalenga kufikisha ujumbe
alioukusudia hususani kwa baadhi ya watu wanaomuwekea mipango mibaya ya
kuharibu kazi zake za kimuziki
Alisema kuwa wapo baadhi ya washika dau wanaojikita katika maswala ya
muziki kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wakimnyonya mwanamuziki
bila ya kujali jasho lake na nguvu yake kwa kazi anayoifanya
Kutokana na hali ya kunyonywa wasanii na washika dau hao alisema
msanii atakapopata akili na kuwa na uwezo wa kugundua kuwa ananyonya na
hawezi kufika mbali hali inabadilika kwa kuanza kukandamizwa na kuwekewa
vikwazo katika kazi zao
“Baadhi ya washika dau wanawaogopa wasanii wakubwa kwa kuwa tishio
katika biashara zao hivyo hata wasanii wachanga pia wananyimwa nafasi ya
kukua kisanii kwa kuhofia kuja kuwageuka baadaye pindi watakapopata
nafasi ya kufanya hilo” alisema Gadna
Aliongezea kuwa mfumo wa muziki hauko sawa na upo kwa lengo la
kumnyonya msanii hali ambayo inazidi kudidimiza wasanii na muziki wa
nchi hii hali inayosababisha muziki unakuwa kwa kusikilizwa redioni na
si kwa kukuwa kwa kipato kwa wasanii
Alisema kuna hujuma zinazoendelea kwenye soko la muziki zenye lengo
la kumnyonya mwanamuziki na kumpa utajili mdau wa muziki sababu hiyo
inapelekeea wanamuziki wa nchi yetu kutoendelea katika soko la muziki
Lady JayDee hivi karibuni amekuwa akitumia mtandao wa Twitter kwa
ajili ya kutuma ’tweets’ zenye ujumbe kwa mtu aliyemkusudia ingawa
hazikuonyesha wazi wala kutaja jina la muhusika.
SUGU a.k.a Mr2 ambaye kwa sasa ni mbunge wa kuchaguliwa wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Mbeya Mjini ambaye anachukuliwa kama MFALME na MUASISI wa muziki wa kizazi kipya Tanzania na Afrika mashariki ndiye alikuwa wa kwanza kabisa kulalamikia hili suala la mfumo wa unyonyaji wa muziki Tanzania na wanaouendesha huo mfumo aliwataja waziwazi kwenye vyombo vya habari,mtaani,Bungeni na hata kwenye kitabu chake kinachoitwa 'From Street to the Parliament'.
Lady JayDee
Sasa kama kama Mfalme mheshimiwa SUGU aliongea halafu MALKIA Judith Wambura a.k.a lady JayDEE naye anaongea suala hilohilo hapo sidhani kama mtu hata kama haujui kusoma je hata picha hauioni?
Mfumo huo ni lazima ufumuliwe na wa kuufumua ni nani?
Mh.SUGU siku aliyokuwa akila kiapo Bungeni Dodoma