Gadner G Habash ambaye ni Meneja na
Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, amezungumza juu ya
maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni
maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia
kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa,
basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na Lady Jay
Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la wimbo
kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu
kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na
wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya
Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema lakini
siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio
akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake
nitakufa kisabuni.
Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa
halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama
watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu
wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu
kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma
sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona
kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo
Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina,
ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado
alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda
sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona
umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye
grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio
sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.
Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni
ya redio inategamea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla
kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata
hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila
tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari
fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu
wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani
lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa
madhara nisiposema.
Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine
unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema
adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga
wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu
waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu
walisimama hawakuogopa. Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru,
kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la
kawaida kuogopa,lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili
mradi useme ukweli, basi inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu
yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea
kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli
na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee
kukosea wabadilikee….
Mwisho..!
Jide kawa kinega wa kike
ReplyDelete