Mbeya, 29 Aprili 2025 – Kongamano kubwa la mafundi lilioandaliwa na FundiSmart chini ya uongozi wa Mkurugenzi Fredy Herbert Pole limefanyika kwa mafanikio makubwa, likihudhuriwa na zaidi ya washiriki 2,000 kutoka sekta mbalimbali za kiufundi na mnyororo mzima wa thamani wa kazi za ufundi nchini Tanzania.
UBUNIFU NA UONGOZI MADHUBUTI WA NDUGU FREDY POLE
Mafanikio haya yametokana kwa kiasi kikubwa na uwezo wa ndugu Fredy Pole kuongoza kwa ubunifu unaoleta matokeo chanya kwa jamii. Fredy amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mafundi wanapata nafasi ya kuonekana, kuunganishwa na fursa, na kubadilika kwenda kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi.
Katika maandalizi ya kongamano hili, alihusisha makundi mbalimbali
wakiwemo:
- Vijana aliowalea na
kuwapa ujuzi, ikiwemo katika sekta ya media
- Wadau wa biashara
na maendeleo aliyewahi kushirikiana nao
- Watu wenye
ushawishi katika jamii
- Mafundi wa fani
mbalimbali
- Wafanya biashara
- Serikali
- Vyombo vya habari
- Washiriki walioko kwenye mafunzo ya ufundi
MALENGO YA FUNDISMART
Katika hotuba yake, ndugu Fredy Pole alieleza malengo makuu ya
FundiSmart kuwa ni:
- Kuwaunganisha
mafundi na fursa za kazi, zabuni na mitaji
- Kuanzisha application
ya mafundi kwa ajili ya masoko na mawasiliano
- Kusaidia mafundi
kurasimisha taaluma zao kwa kushirikiana na taasisi kama VETA
- Kushawishi taasisi za kifedha kuwatengenezea mafundi huduma mahsusi
CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI MAFUNDI
Fredy pia aligusia changamoto kadhaa zinazowakabili mafundi, ikiwemo:
- Gharama kubwa za
kupata vyeti vya VETA
- Ukosefu wa huduma
maalum za kifedha kwa mafundi
- Kutokuaminiwa kwa mafundi wazawa kwenye zabuni za serikali
KAULI ZA WADAU MUHIMU
MRATIBU WA VETA
- Alisisitiza mafundi
kufanya kazi kwa uadilifu na weledi
- VETA ipo tayari
kusaidia mafundi kurasimisha kazi zao
- Gharama za usajili
wa ujuzi zitapitiwa upya ili zisiwe kikwazo
MKUU WA WILAYA YA MBEYA JIJI
- Aliwataka mafundi
kuwa waaminifu na wachukue tahadhari kazini
- Aliahidi kufanyia
kazi changamoto ya leseni za kazi na usajili kupitia EURA
- Alipendekeza OSHA
washirikishwe katika makongamano yajayo
- Alihimiza mafundi
kuwa na bima za afya
- Alitoa wito kwa
taasisi za kifedha kuunda huduma rafiki kwa mafundi
- Aliwahimiza mafundi kuwapa thamani wadhamini wa kongamano
WADHAMINI WAKUU: LODHIA INDUSTRIES
Kampuni ya Lodhia Industries Ltd, ambao ndio wadhamini wakuu wa kongamano, walitoa fursa kwa mafundi kushirikiana nao kwa karibu zaidi. Wamefungua milango kwa mafundi kutembelea kiwanda chao kwa mafunzo, ushauri, na kuibua fursa mpya kupitia jukwaa la FundiSmart.
HITIMISHO
Kongamano hili limekuwa ni chachu ya mabadiliko makubwa kwa sekta ya
ufundi Tanzania. FundiSmart imejidhihirisha kuwa daraja la kweli kati ya
mafundi, soko la ajira, na taasisi mbalimbali za maendeleo. Ni dhahiri kuwa
mafundi wa Tanzania sasa wana jukwaa sahihi la kuinua taaluma zao.
“FUNDI HUU NI
WAKATI WAKO WA KUWA FUNDISMART!”
0 comments:
Post a Comment