Monday, 5 May 2025

MIXING DOCTOR AWANIA TUZO MBILI KWENYE TANZANIA GOSPEL MUSIC AWARDS 2025

Katika tasnia ya muziki wa Injili, kuna majina machache yanayojitokeza kwa ubora, ubunifu, na uaminifu katika utumishi. Moja ya majina hayo ni Mixing Doctor kutoka Music Surgery, ambaye kwa neema ya Mungu amepata nafasi ya kipekee ya kuwania Tuzo Mbili katika Tanzania Gospel Music Awards (TGMA) 2025.

Kwa mwaka huu, Mixing Doctor ameteuliwa katika vipengele viwili muhimu vinavyohusu upande wa uzalishaji wa muziki:

  1. Muandaaji Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka
  2. Mtayarishaji Bora wa Sauti wa Muziki wa Injili wa Mwaka

Hili ni jambo la kujivunia si tu kwa Mixing Doctor binafsi, bali pia kwa wadau wote wa muziki wa Injili nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Ubunifu wake wa kipekee na kazi bora alizozifanya kwa wasanii wengi wa Injili zimempa nafasi hii ya pekee.

NAMNA YA KUPIGA KURA

Ikiwa unataka kumuunga mkono Mixing Doctor na kuonyesha kuthamini kazi yake nzuri, fuata hatua hizi rahisi kupiga kura:

  1. Tembelea akaunti ya Instagram ya @mixingdoctor au @tanzaniagospelmusicawards
  2. Bonyeza link iliyopo kwenye bio – itakupeleka kwenye ukurasa wa kupiga kura
  3. Chagua kipengele cha "Production and Technical Awards"
  4. Tafuta na chagua vipengele viwili:

-          Muandaaji Bora wa Sauti wa Muziki wa Injili wa Mwaka

-          Mtayarishaji Bora wa Muziki wa Injili wa Mwaka

  1. Katika kila kipengele, chagua jina Mixing Doctor
  2. Bonyeza Click to Vote chini ya picha yake
  3. Ukiona ujumbe “You have voted for Mixing Doctor”, basi kura yako imepita salama.

Uteuzi huu ni ushuhuda kwamba kazi njema haipotei bure. Mixing Doctor ameendelea kuwa msaada mkubwa katika kuboresha viwango vya uzalishaji wa muziki wa Injili na sasa anatambuliwa kitaifa.

Tuna nafasi ya kumuwezesha kushinda kwa kumpigia kura. Tupige kura, tushirikishe wengine, na tuendelee kuombea mafanikio ya huduma hii.

Mungu akubariki sana kwa msaada wako.

0 comments:

Post a Comment