1. HIFADHI TIKETI YAKO VIZURI
Hakikisha
umeiweka tiketi yako mahali salama, iwe ni tiketi ya kawaida, VIP, Special
Seat, au Meza ya watu 5. Ikiwa ni e-ticket, screenshot au print
nakala ili kuepuka matatizo ya mtandao siku ya show.
2. PANGA MUDA WAKO – FIKA MAPEMA ⏰
Show inaanza
saa 12:30 jioni na itaendelea hadi saa 5:59 usiku. Kufika mapema
kutakusaidia:
- Kuepuka
foleni ndefu
- Kupata
nafasi nzuri ya kukaa (kwa wale wa Regular Tickets)
- Kujipanga
kwa ajili ya burudani kamili
3. VAA MAVAZI MAZURI NA YALIYO NA MWELEKEO WA VICHEKO
Hii ni show
ya kipekee, hivyo vaa kitu ambacho kinakufanya ujisikie huru na unaelekea
kwenye tamasha kubwa! Ikiwa uko kwenye Regular, VIP au Special Seat,
unaweza pia kwenda na muonekano wa kimaridadi kidogo kwa vibes nzuri.
4. ENDA NA MOOD YA KUCHEKA – USILETE STRESS!
Hii ni siku
yako ya kufurahia na kicheko, kwa hiyo jiandae kwa burudani ya kiwango cha juu!
Pumzika, acha stress zote nyumbani, na ujue kuna vichekesho vitakavyokufanya
usahau matatizo yote kwa muda!
5. NJOO NA MARAFIKI AU FAMILIA – BURUDANI NI TAMU ZAIDI KWA PAMOJA!
Kama una
nafasi ya kuja na rafiki au ndugu zako, itakuwa bomba zaidi! Meza ya watu 5
bado inapatikana, kama unataka kufanya booking ya kifamilia au na washikaji.
6. SHIRIKI NA WENGINE KWENYE MITANDAO!
Usisahau
kushare excitement yako! Post kuhusu show, tumia hashtag kama:
#EasterComedyShowMbeya
#NjooUchekeMpakaMbavuZiiume
#StandUpComedyMbeya
Pia,
fuata ukurasa wa Instagram kwa updates zote za mwisho @standupComedy_mbeya
7. KUWA TAYARI KWA SUPRISE NA BURUDANI ZAIDI!
Mbali na
vichekesho, kutakuwa na burudani nyingine za muziki, michezo midogo, na
surprises kutoka kwa waandaaji! Jiandae kwa kitu spesho ambacho hakijatangazwa
bado!
Siku
inakaribia! Tunakutana TUGHIMBE HALL kwa show kali ya Pasaka!
Onhoo Safi Ngoja niishi vizuri na Matajiri sio ya kukosa hioo!
ReplyDelete