Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Friday, 31 May 2013

UZINDUZI WA TUMANYENE SOCIAL HALL WAAHIRISHWA

Afisa mipango na matukio

Uzinduzi wa ule Ukumbi mpya na wa kisasa kabisa wa burudani jijini Mbeya (GreenCity) unaokwenda kwa jina la Tumanyene Social Hall uliokuwa ufanyike tarehe 02/06/2013 umeahirishwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Afisa mipango na matukio wa

Monday, 20 May 2013

HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014- MH JOSEPH O. MBILINYI (MB)


(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’

Mheshimiwa Spika,

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!



2. UHURU WA UHARIRI NA USALAMA WA WANAHABARI

Mheshimiwa Spika,

Kwa masikitiko makubwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalitaarifu Bunge lako tukufu kwamba sasa Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya fedheha (The List of Shame) ya mataifa ambayo taaluma ya habari ni taaluma ya hatari kwa wale wote wanaoitumia kama sehemu ya wajibu wao kwa taifa na kama ajira yao. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari Ulimwenguni (the Committee to Protect Journalists - CPJ) iliyotolewa mwaka huu 2013, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPJ mwaka 1992, Tanzania imeingizwa kwenye orodha ya nchi 20 ambazo ni hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kutokana na hatari ya kuuwawa kwa mwaka 2012 (20 Deadliest Countries in 2012). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilishikilia nafasi ya 7 ulimwenguni kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa kuhatarisha maisha ya waandishi wa habari.

Sunday, 12 May 2013

Official!!TUMANYENE SOCIAL HALL KUZINDULIWA TAREHE 02 June


Ule ukumbi wa burudani wa kisasa kabisa jijini Mbeya uliopo eneo la Nzovwe utazinduliwa tarehe 02/06/2013 ukiambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakubwa na wanaochipukia.
Akizungumza na safu hii Afisa uhusiano wa

Friday, 10 May 2013

BIBI KIZEE AHAMIA CHADEMA

Imeandikwa na Mango Pickle
BIBI AMEAMIA CHADEMA
BAADA YA KUAMBIWA KUWA CCM NI YA FAMILIA ZIFUATAZO
1.LOWASSA
2.MKAPA
3.KINANA
... 4.CHENGE
5.MWINYI
6.KARUME
7.ROSTAM
8.SITTA
9.MRAMBA
BIBI ALIPOGUNDUA FAMILIA YAKE HAIPO, NIKAMWAMBIA HAWAKUJUI
HIVYO TUSIO CCM WOTE TUKO CHADEMA,
BIBI ALITUPA KILEMBA CHA CCM NAKUOMBA SKAFU NILIYOKUWA NIMEVAA NA KUMPA
UKOMBOZI NI SASA

Source jamiiforums 'Mango Pickle'

Friday, 3 May 2013

MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA,

MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)

KUHUSU

MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2013/2014
(Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)



UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imeanzishwa kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Waraka wa Rais uliochapishwa kama Tangazo la Serikali Na. 494 la tarehe 17 Desemba 2010. Majukumu ya Ofisi hii yameainishwa katika Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2010 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2010) lililochapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 494A la tarehe 17 Desemba 2010. Kwa mujibu wa Nyongeza ya Pili ya Tangazo hilo, pamoja na mengine, Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imekasimiwa majukumu ya masuala ya kikatiba, uendeshaji na utoaji wa haki, uendeshaji mashtaka na haki za binadamu. Kwa sababu ya matukio ya hivi karibuni yanayohusu utendaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mchakato wa Katiba Mpya na kwa kuzingatia umuhimu wake katika mustakbala wa taifa letu, tunaomba kuanza na masuala yanayoihusu Tume na uendeshaji wake wa mchakato huo.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mheshimiwa Spika,

Katika mwaka wa fedha 2012/2013, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 33.944 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kwa mujibu wa Maelezo ya Makadirio ya Matumizi Mengineyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 yaliyoletwa mbele ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala mwezi uliopita, hadi kufikia tarehe 25 Februari, 2013 Tume ilishapokea shilingi bilioni 18.473 kutoka Hazina na ilikwishatumia shilingi bilioni 14.968, sawa na 81% ya fedha zilizopokelewa. Kwa mujibu wa Maelezo hayo, shilingi bilioni 3.504 ambazo hazijatumika zimetengwa kwa ajili ya kulipia madeni kutokana na huduma za uchapishaji wa Mwongozo wa Mabaraza ya Katiba, uratibu wa mchakato wa kupatikana Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba na gharama nyingine za uendeshaji wa Ofisi.

Maelezo ya Tume yanaonyesha kwamba shillingi bilioni 15.471 ambazo hazijatolewa na Hazina zitatumika kwa ajili ya kusambaza nakala milioni moja za Rasimu ya Katiba Mpya (shilingi bilioni 3.848); elimu kwa umma juu ya Rasimu ya Katiba Mpya (shilingi milioni 400); kuratibu na kuendesha Mabaraza ya Katiba kwa nchi nzima (shilingi bilioni 4.734); na shilingi bilioni 6.488 kwa ajili ya matumizi mengine pamoja na ‘stahili za Wajumbe na Sekretarieti.’

Mheshimiwa Spika,

Katika Maoni yetu ya mwaka jana, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ililalamikia kile ilichokiita “... matumizi yasiyoelezeka na yasiyokubalika ya fedha za umma hasa hasa katika mazingira ambayo wananchi wanahubiriwa na watawala kwamba miradi ya maendeleo yao ya kiuchumi na kijamii haitekelezeki kwa sababu ya ufinyu wa bajeti ya Serikali.” Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilidai kwamba shilingi bilioni 14.633 zilizotengwa kwa ajili ya kuwalipa wajumbe na watendaji wa Tume posho mbali mbali zilikuwa zinatishia kuigeuza “heshima ya kutumikia waliyopewa wajumbe wa Tume kuwa hongo ya Serikali.” Madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuitaka Serikali ieleze Bunge hili tukufu gharama zote za kila Mjumbe wa Tume, Sekretarieti na watumishi wengine wote wa Tume “ili Wabunge na wananchi wa Tanzania wafahamu kodi wanazolipa zinavyotumika katika mchakato wa Katiba Mpya” yalikataliwa na Serikali kwa hoja kwamba taarifa hizo ‘ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa.’

Mheshimiwa Spika,

Bunge lako tukufu linaombwa kuidhinisha shilingi bilioni 33.944, kiasi kile kile kilichoidhinishwa mwaka jana, kwa ajili ya matumizi ya Tume kwa mwaka wa fedha 2013/14. Kiasi hiki ni pamoja na shilingi bilioni 12.193 kwa ajili ya “... kulipia posho za vikao kwa Wajumbe wa Tume 34 na Sekretarieti 160 ...”; shilingi bilioni 1.728 ambazo “... zitalipia posho ya kujikimu kwa ajili ya Wajumbe na Sekretarieti wanaposafiri ndani ya nchi kikazi”; na shilingi bilioni 1.650 kwa ajili ya “... kulipa gharama za nyumba za Wajumbe na Sekretarieti wanaotoka nje ya Dar es Salaam.”

Aidha, kuna shilingi milioni 18 zinazoombwa “... kwa ajili ya kugharamia chakula kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti watakaokuwa wamepata maambukizi ya ukimwi”;

Tuesday, 30 April 2013

CHADEMA WAFUNGUKA IRINGA

Baada ya mkutano waliofanya Mwanza Wabunge wa Chadema walio fukuzwa bungeni kwa madai ya utovu wa nidhamu  wamefanya mkutano jimbo la Iringa mjini ili kushtaki kwa umma uonevu walio fanyiwa.

Hapa ni yanayojiri mkutanoni.

• Diwani wa Iringa mjini, Nyalusi, wananchi wa Iringa wana imani na viongozi wa CHADEMA, kuliko walioko madarakani. Kapanda Sugu

• Sugu: Tutaendelea kukomaa. Kiti kinamfukuza Lissu kwa kufanya kazi yake, wakati Serukamba mbunge wa FT, akiachwa! Tusi kubwa, hakuna mbunge katika jumuiya ya madola amewahi kutukana tusi baya kama hilo, limevunja rekodi Jumuiya ya Madola

Thursday, 11 April 2013

HILI NI JANGA


HII RIPOTI IMENISIKITISHA SANA

Wasichana wa Nzovwe jijini Mbeya wanapenda kupigwa 'mtungo'

WASICHANA wa eneo la Nzovwe, jijini Mbeya wametuhumiwa kushinda katika klabu za kuuza pombe za kienyeji, hasa nyakati za usiku na kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja kwa siku kwa tamaa ya fedha.

Imedaiwa tabia ya wasichana hao, kupenda kuomba fedha kwa wanaume tofauti wanaokuwa wanakunywa pombe katika klabu hizo, hupelekea mwisho wa siku wakubali kufanya ngono zembe na mwanaume zaidi ya mmoja.

Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na wakazi wa eneo hilo, katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Vijana Mabalozi Watanzania wanaoishi na virusi vinavyosababisha Ukimwi (TAYOPA).

Mkoa wa Mbeya ni wa nne kutembelewa na TAYOPA ambao wapo kuutambulisha mradi wao uitwao 'Vijana Tuzinduke ili kujikinga na Ukimwi'.

Tuesday, 2 April 2013

Elly na Mlimani Youth Group

                Hapa ELLY (aliyevaa t-shirt nyeupe) akiwa na member wa Mlimani Youth Group

KIASHIRIA KIKUU CHA GREENCITY

                                              KIASHIRIA KIKUU CHA GREENCITY

Programu za organisation ya EGY BUSINESS SOLUTION na MLIMANI YOUTH GROUP

Programu za organisation  ya EGY BUSINESS SOLUTION na MLIMANI YOUTH GROUP walipotembelea  kituo cha watoto yatima IWAMBI-Organisation hii inaongozwa na kijana mdogo tu ambaye ni mfano wa kuigwa katika jamii hii ya kizazi cha sasa,kijana huyu anakwenda kwa jina la Elly Lawi-BONKE.

Programu za organisation ya EGY BUSINESS SOLUTION na MLIMANI YOUTH GROUP

Programu za organisation  ya EGY BUSINESS SOLUTION na MLIMANI YOUTH GROUP walipotembelea  kituo cha watoto yatima IWAMBI-Organisation hii inaongozwa na kijana mdogo tu ambaye ni mfano wa kuigwa katika jamii hii ya kizazi cha sasa,kijana huyu anakwenda kwa jina la Elly Lawi-BONKE.