Saturday, 11 November 2023

PRODUCER MICKMER NI KURUNZI YA PRODUCTION ILIYOMULIKA KILA AINA YA MUZIKI AKIWA NA UMRI MDOGO SANA AKAWALAZA NA VIATU MANGULI ‘Atunukiwe Plaque maalum’


South side music mick mick mick mickmerr umri unakwenda miaka inasogea na kifo kinasogea… hivyo ndio wimbo wa mtafya unaitwa JE UMEJIPANGA unavyoanza kusikika nashtuka narudia tena kusikiliza jingo kwa umakini Zaidi sikio langu linaridhika kuwa nilichokisikia ndivyo kilivyo ‘South side music mick mick mick mickmerr’ nashtuka na kuingia mashaka kidogo kama huyu ninayemsikia ndio huyu Mickmerr producer ninayemfahamu mimi nikilinganisha umri alionao sasa na kama yeye ndiye aliyetengeneza huu wimbo kipindi kile na kama ni yeye je kipindi hicho umri aliokuwa nao na ukubwa wa ngoma husika ndipo nikaamua kuchukua jukumu la kutaka kupata uhakika kwa kumpigia simu.
‘Grrr grrr grrr’
Mwandishi: Micky mambo vipi?
Mickymer: Poa,inakuaje?
Mwandishi: Mungu mwema anatupigania,sorry hapa nilikuwa nasikiliza wimbo wa Mtafya unaitwa je umejipanga umetoka zamani kidogo kama sikosei ni mwaka 2012 au 2013 hivi na nimesikia kwenye wimbo huo jingo lako,vipi hii imekaaje?
Mickymer: ni mimi niliitengeneza hiyo nyimbo
Mwandishi: Hongera sana,hii habari imenishtua sana,kipindi wimbo huu unatoka miaka hiyo kama sikosei ulikuwa kidato cha pili au tatu sasa ilikuwaje kwa umri huo ukaweza kutengeneza hit song kama hiyo na ulijifunzaje funzaje kwa umri huo?
MickMer: Sikuanza kama producer na sikuwa na ndoto ya kuwa producer,ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mwanamuziki na tulikuwa na Crew yetu iliyokuwa inaitwa REGISTAA tukiwa shule ya msingi na mimi ndio nilikuwa kiongozi. Kipindi hicho tulikuwa tunapenda sana kuimba sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye vipindi vya watoto redioni pale Mbeya fm na Generation fm,kwenye sherehe mbalimbali tulikuwa tunavamia tu bila kualikwa tunaimba pale ili mradi kujifurahisha kwasababu tulikuwa tunapenda (kwenye sherehe kama kama kipaimara na ubatizo,harusi n.k)  huu wimbo tuliimba wawili kutoka kwenye crew yetu na Fam Jizzo
Mwandishi: Endelea….
Mickmer: Tukiwa bado shule ya msingi tulifanikiwa kurekodi wimbo wetu wa kwanza kwa Producer Gwamaka Kameta (aliyetengeneza wimbo wa masanja – Kemea pepo) uliokuwa unaitwa DUNIANI na wimbo ulipigwa sana redioni na kutuongezea sana morali ya kuendelea kufanya muziki mpaka ikatupelekea kurekodi wimbo wetu wa pili kwa mtayarishaji Obbymack David alikuwa na geto studio ngoma yetu iliitwa SCHOOL.
Mwandishi: Nini kilifuata….
Mickmer: Baada ya kumaliza darasa la saba 2008 ilikuwa ni bize tu na muziki no dili no ishu yoyote hapo baadaye likanijia wazo la kuanza kujifunza kutengeneza muziki na katika kuanza kwangu kutengeneza sikufundishwa na mtu yoyote na hakuna mtu ambaye atakuja kusimama na kusema yeye kanifundisha muziki
Mwandishi: Ulianzaje sasa Uproducer?
Mickmer:Baada ya kurekodi hizo kazi kadhaa za muziki nikawa nimeona program wanayotumia (FL studio) basi na mimi nikaitafuta na kuanza kuichezeachezea na kumbuka hapo hatuna computer ila nilikuwa naenda library na jamaa zangu ingawa wenyewe hawakuzingatia sana tunalipia buku kwa lisaa then saa ikiisha naondoka mpaka siku nyingine. Muda ukaenda sana mpaka siku nilipokutana na brother Wiseman
Mwandishi: Wiseman ni nani?
Mickmer: Sitaweza kumsahau Brother Wiseman kwenye maisha yangu yote ya uandaaji wa muziki kwasababu huyu brother ndiye alinipatia fursa ya kuweza kukiendeleza kipaji changu. Ilikuwa hivi ‘Wiseman alikuwa na studio yake,kuna siku alisikia biti yangu ambayo ilikuwa trap aliipenda na kunikaribisha studio kwake na kunikabidhi niitumie kwa chochote kile bila kulipia hata senti na wakati mwingine alikuwa ananiachaia freely kabisa hata asipokuwepo,alinipao uhuru wote hapo ndipo ujuzi wangu ulikuwa mara dufu’.
Baada ya kujipika sana kwa Wiseman nikajiona sasa ninaweza kuwa producer sasa wa kuweza kuwatengenezea wasanii nyimbo rasmi basi nikaenda kwenye studio moja hivi kwa ajili ya kufanyakazi wakanipokea vizuri na pale kulikuwa na maproducer wazambia nikawa nafanya kazi pale ila wale maproducer wa pale wakawa wananitenga basi nikaamua kupiga chini na kutafuta mahali pengine.Baada ya siku kadhaa kuna jamaa akaniambia pale SouthSide wanatafuta producer so nikaamua kwenda pale na nikakutana na Danz
SOUTH SIDE MUSIC
Nilipofika South Side pale nikakutana na DANZI akanifanyia interview na wasananii watano kwa kuwarekodi na baada ya kumaliza nikajibiwa pale pale kuwa nimefaulu na kazi nimepata nikapangiwa siku ya kuanza kazi. 
Siku niliyopangiwa kuanza kazi nikafika na nikamkuta mtu mwingine aliyejitambulisha kuwa yeye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa pale na akajitambulisha kwa jina la Aggrey.Aggrey akaniambia kuwa pale producer yupo ila basi akanifariji kwa kunipangia tarehe tofauti tofauti mpaka nikakata tamaa nikaacha kwenda. Muda ulipita sana nikawa kuna studio naitwa kama deiwaka tu mpaka siku niliyokuja kukutana kwa mara nyingine na Aggrey mtaani tu na kuanza kunishawishi niende studio. Nakumbuka siku hiyo maeneo ya Mwanjelwa tulikuwa tunahamisha vifaa kwenye saloon ya dada yangu ndipo tukakutana na Aggrey akaniambia we dogo tunakutafuta sana uje tufanye kazi ila nilimkatalia sana katakata kwasababu nilikuwa tayari nina kinyongo naye lakini alinibembeleza sana mpaka dada yangu akamsaidia kunishawishi hadi nikakubali.

KUINGIA SOUTH SIDE MUSIC
Mwaka 2011 naingia pale studio nilikuta studio imelala kabisa imepitwa na studio zote hapa mjini kwasasa (akazitaja kwa majina),mimi nataka tuirudishe hii studio kwenye ramani na naamini kwa uwezo wako wa utayarishaji tukichanganya na uwezo wangu wa kiutawala tutarudi kwenye nafasi yetu. Basi Aggrey pale pale akagawa majukumu yakwake na yakwang kama ifuatavyo:-
MAJUKUMU YANGU
Kutengeneza muziki mzuri
Mahusiano mazuri na wasanii
Kupata wasanii wakali
MAJUKUMU YAKE
Kufanya promotion
Mahusiano mazuri na media
Kufanya masoko
Kupata wasanii wakali
Kubuni contents
Rasmi tukaanza kufanyakazi na pale studio baadhi ya wasanii niliowakuta pale ni pamoja na DavyStar,Zax 4Real,Berdon n.k
KUFANYAKAZI NA MTAFYA
Kuna siku nilikuwa napita Mabatini nikamkuta Mtafya anaimba imba tu mtaani nikaona huyu mbona mkali na hastahili kufanya kimtaani taani ila kumfuata kumuambia nikawa  siwezi kumfuata ukizingatia umri wangu ulikuwa mdogo sana pia nina hali Fulani hivi ya kushindwa kumfuata mtu moja kwa moja,nikamshtua DavyStar coz niliamini yeye atamuweza na kweli Davy alimcheki na kumleta studio Mtafya na kumjumuisha kwenye familia ya SouthSide music na chap kwa haraka tukapiga mkono mmoja tu uliokwenda kwa jina JE UMEJIPANGA ambao ndio ulifungua rasmi njia ya Mtafya kwenye harakati zake za muziki.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2012 tukawa tayari tumeiteka Mbeya nzima kama vile malengo yetu ambayo tulikuwa tumeyaweka na boss wangu Aggrey.
Mimi ndio producer ambaye nimefanyakazi na wasanii wote wa kizazi cha kati kile cha miaka ya 2012 mpaka 2013 kuanzia Zax 4Real,Berdon,DavyStar,Mtafya,Star boy (Piano),Samicho n.k 
Mwaka 2013 niliondoka Mbeya na kwenda dar es salaam kwa ajili ya kusoma na mishe zingine na kule nikafanikiwa kufanya kazi na maproducer na wasanii wakubwa sana ila sitaweza kuzitaja kwasababu hazina manufaa yoyote kwangu coz nilifanya kama kivuli tu.
Nje ya SOUTH SIDE MUSIC nimeshafanyakazi sehemu zingine tofauti tofauti:-
T-Motion Music – Pale wakati wanaanza anza walinichukuwa kwa ajili ya kuenda kuwapa ujuzi Zaidi na nikafanikiwa kuwatengenezea nyimbo kadhaa za Gospel na Bongo Fleva kama nne tano hivi naweza kuzitaja baadhi:-
Natamani – Meshamazing
Milele – Meshamazing
Natural woman – Ammy Chiba x Zax 4Real x Anno Melody x Fide Losso x Meshamazing
Sarafina – Zax 4Real 
Access Fm Redio – Pale nilifanya nafasi ya Redio producer
Kwa sasa natarajia kufungua studio yangu mwenyewe very soon na I promise you nyie ndio mtakuwa wa kwanza kuifahamu
KUHUSU AGGREY SOUTH SIDE
Kwa kifupi sana ‘Aggrey kwangu alikuwa ni Zaidi ya Boss Zaidi ya brother Zaidi ya mlezi Zaidi ya mshirika’

Kupitia mazungumzo haya nimegundua kuwa Mickmer: 
Ni producer aliyewatengeneza wasanii wengi sana Mbeya walionza kujulikana kwenye Generation ya 2012 na kuendelea
Hapendi na hataki kuwazungumzia wasanii ambao tayari wametoka kuwa yeye ni sehemu ya njia iliyowafikisha walipo ila kama kuna msanii atahisi kuna mchango wowote kutoka kwake yeye ndio aseme
Anaheshimu sana jitihada na kazi za producers wengine
Anapenda kule vipaji
Baadhi ya wasanii aliowahi kufanya nao kazi kwa nyakati tofauti tofauti ni Meshamazing,Annomelody,Zax 4Real,Berdon,Star Boy (Piano),Raymond (Rayvan),Danzi,DebbyCulture,Samicho,Mtafya,DavyStar na wengine

Mickmer ni versatile producer yaani chochote unachotaka anakupa iwe gospel,hiphop,bongofleva,zouk,R&B,Afro pop,singeli n.k
HipHop – Je Umejipanga – Mtafya
African zouk – Natural woman – AmmyChiba x Zax x Meshamazing x FideLosso X Anno Melody
Afro pop – Sarafina – Zax 4Real
BongoFleva – Milele – Meshamazing
N.k

Timu nzima ya Burudani Mbeya inampongeza sana na kumtakia mema kila analolifanya katika kuipeleka mbele Sanaa ya mkoa wetu.

3 comments:

  1. Mbeya Vichwa NI vingi Sana kwenye sanaaa kwa KILA angle mkuu wangu mapiano yaendeleee
    Hongera kwa mmoja anaepambania hiii sanaaaa mbeya

    ReplyDelete
  2. Mickmery kijana mmoja mnyenyekevu sana! Mungu amfungulie milango zaidi binafsi namuona mbali sana🙏❤️

    ReplyDelete