Tuesday, 30 April 2013

CHADEMA WAFUNGUKA IRINGA

Baada ya mkutano waliofanya Mwanza Wabunge wa Chadema walio fukuzwa bungeni kwa madai ya utovu wa nidhamu  wamefanya mkutano jimbo la Iringa mjini ili kushtaki kwa umma uonevu walio fanyiwa.

Hapa ni yanayojiri mkutanoni.

• Diwani wa Iringa mjini, Nyalusi, wananchi wa Iringa wana imani na viongozi wa CHADEMA, kuliko walioko madarakani. Kapanda Sugu

• Sugu: Tutaendelea kukomaa. Kiti kinamfukuza Lissu kwa kufanya kazi yake, wakati Serukamba mbunge wa FT, akiachwa! Tusi kubwa, hakuna mbunge katika jumuiya ya madola amewahi kutukana tusi baya kama hilo, limevunja rekodi Jumuiya ya Madola


• Sugu: Kauli ya WASSIRA, Kibanda ni nani? Ubinadamu na utu kwao ni cheo!

• Kiwia: Matusi kwa Wtz ni kufanywa maskini katika nchi tajiri, akina mama kwenda na nyembe na kila k2 kujifungua, kuzungumzia madawati miaka 50 ya uhuru wakati Kenya wanazungumzia kompyuta kwa kila mtoto.

• Kiwia: Ukiona mahali kuna amani ya kweli inayotokana na haki pamoja na demokrasia, ujue kuna watu wachache wamejitoa, ikibidi kwa jasho na tone la damu! Bunge sasa limegeuzwa kuwa rubber stamp ya masuala ya CCM!

• Mnyika anasema fedha za DECI zirudishwe. Wabunge wanazuiwa kujadili suala la Deci eti liko mahakamani, mbona Magufuli aliamua kuongelea suala la samaki wake kwani aliwagawa hao samaki wakati kesi ikiendelea.

• Mnyika anatuma salamu kwa Kamhanda kuwa alisababisha mauaji ya Mwangosi. Anasema kitendo hiki hakivumiliki na hawataliacha suala hili bila hatua kuchukuliwa

• Wenje anazungumzia suala la watoto kukaa chini kwa kukosa madawati wakati mbao zinasafirishwa kwenda nje kila siku kwa dili za wakubwa.

• Wenje anasema Maige aliwajibishwa kwa upotevu wa twiga wawili iweje kwa kawambwa ishindikane?

• Suala la mfumuko wa bei na kodi zisizo za lazima. Wenje "Kama akina Lusinde ndio washauri wa serikali hasa kupandisha thamani ya pesa zetu eti kwa kuondoa picha ya nyoka na kuweka ya Nyerere na Karume basi tumeruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa".

• Dr Slaa Anasema wabunge wake hawatatafuna maneno inapofika suala kuiwajibisha na kuiagiza serikali kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

• Anasema Serikalii hii ni IMPOTENT kuanzia yule wa juu hadi walioko chini.

• Ameagiza; wabunge wa CHADEMA wakaze mwendo kuwa more focused na wakali zaidi kuliko sasa, kama kiti kinaendelea na tabia ya kuminya haki.

• Ameagiza kuanzia sasa hotuba zote za Kambi ya Upinzani Bungeni zitolewe nakala na kugawiwa hadi ngazi ya kata ya chama, kupeleka taarifa na maarifa kwa wananchi, Watanzania kila mahali nchi nzima.

• Mkutano umekwisha kwa amani, wananchi wanaandamaa kwa amani wakilisukuma gari la Dr Slaa na kuimba "Raisi, raisi, raisi, ....

0 comments:

Post a Comment