Tuesday 30 April 2013

Prof. Jay AFYATUKIA SERIKALI

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule, a.k.a Profesa Jay, ameijia juu Serikali katika suala la kusimamia maslahi ya wasanii. Akizungumza katika kipindi cha television kinachorushwa kila siku saa moja na nusu usiku Profesa anasema suala la stika kwenye kazi za wasanii
halipo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii bali ni kwa ajili ya serikali kujipatia mapato ambayo imeona ilikuwa inayakosa kupitia sanaa.Prof anasema 'serikali imeamua kuanzisha suala  stika za TRA bila kuonesha jinsi msanii atakavyonufaika na jasho lake moja kwa moja sana sana mfumo huo unaonesha kuwa utawanufaisha wasambazaji na serikali pekee bila kumuangalia msanii anayeumiza akili yake katika kuhakikisha anatoa kitu kizuri kwa jamii'-anaongea kwa msisitizo.


0 comments:

Post a Comment