Afisa mipango na matukio
Uzinduzi wa ule Ukumbi mpya na wa kisasa kabisa wa burudani jijini Mbeya (GreenCity) unaokwenda kwa jina la Tumanyene Social Hall uliokuwa ufanyike tarehe 02/06/2013 umeahirishwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Afisa mipango na matukio wa
Tumanyene co.ltd ndugu Filbert Eliah amesema sababu za kuahirisha uzinduzi huo umetokana na kikao walichokaa na wadhamini wakuu wa uzinduzi (JEB TECHNOLOGIES & CONSULTANCY ltd) waliopendekeza kupeleka tarehe mbele kidogo ili kufanya uzinduzi huo uwe kwenye kiwango kizuri kitakachoendana na hadhi ya ukumbi wenyewe.
Afisa uhusiano
Afisa uhusiano wa Tumanyene co.ltd ndugu Ezekia anasema uzinduzi huo utakuwa wa aina ambayo haujawahi kufanyika jijini Mbeya na Tanzania nzima.Anasisitiza kuwa siku hiyo hakutakuwa na kiingilio bali kutakuwa na mualiko maalumu tu.STAY TUNED
Sawa tunasubiri
ReplyDeleteKARIBU SANA
DeleteJEB TECHNOLOGIES AU JOB TECHNOLOGIES>?????????
ReplyDeleteJEB TECHNOLOGIES
ReplyDelete