Friday, 31 May 2013

ATHARI 9 ZA VIJANA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA

1. Kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa huondoa utukufu wa Mungu katika ndoa yao
2. Hupunguza heshima katika uchumba na hata katika ndoa baada ya kuoana (maombolezo 1:8)
=mnapofanya tendo la ndoa kabla ya ndoa hupunguza heshima(mchumba
­ wako hawezi kukuheshimu tena, pia huondoa heshima ktk jamii

3. Mkifanya tendo la ndoa kabla ya ndoa mtakuwa mmejenga msingi mbovu wa ndoa yenu...(baada ya kuoana ndoa yenu itaandamwa na migogoro ya ndoa inayohusiana na mapenzi.
MITHALI 6:27-28 anasema "JE MTU AWEZA KUUA MOTO KIFUANI PAKE NA NGUO ZAKE ZISITEKETEE? JE MTU AWEZA KUKANYAGA MAKAA YA MOTO NA NYAYO ZAKE ZISIUNGUE? Bila shaka ataungua

4. Kufanya tendo kabla ya ndoa hupunguza ujasiri wa kuwafundisha na kuwakemea wadogo zetu wanapokose(roho­ itakuwa inakusuta unapomuonya mdogo wako)

5. Kufanya tendo kabla ya ndoa hata kama Mungu atakusamehe lakini bado utabaki na kovu la kudumu

6. Kufanya tendo kabla ya ndoa hubadilisha mwili.(kama ni msichana ubikra utaondoka na hautarudi kamwe maisha yako yote .....HATA UKITUBU VIPI, MUNGU HAWEZI KUKURUDISHIA UBIKIRA

7. Huleta MAZEZE yaani makelele ya ndani.(kila wakati ndani yako kunakuwa na sauti zinazokuambia. Kwanini umefanya hivi, kwanini umefanya hivi na vile. Hayo yanaitwa Mazeze

8. Hupelekea mimba ambazo hazikutarajiwa.
9. Kufanya tendo kabla ya ndoa hudhoofisha mwili na kuharibu ubongo
MITHALI 6:32-33 "MTU AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA AFANYA JAMBO LITAKALOMWANGAM­IZA NAFSI YAKE ATAPATA JERAHA NA KUVUNJIWA HESHIMA WALA FEDHEA YAKE HAITAFUTIKA"

Kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa hupelekea kupata kifo cha kiroho na hata cha kimwili endapo mtaambukizana magonjwa.

0 comments:

Post a Comment