Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es
Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/20114).
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia
amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana
katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu.
Moja ya masharti ya klabu zenye hadhi ya
Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili (U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi
za utangulizi kwenye uwanja wa nyumbani kila timu ya wakubwa
inapocheza.
Mbali ya kuthibitisha timu hizo tatu
kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi imethibitisha rasmi timu tatu
zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa katika mkoa husika. Timu
zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni Small Kids ya Rukwa kutoka
kundi A.
0 comments:
Post a Comment