Friday, 19 September 2025

MUZIKI UNAPOZUNGUMZA: WIMBO MPYA WA MESHACK FUKUTA ‘SILENCE’ WAACHWA HEWANI

‘Meshack Fukuta - Meshamazing (@amazing__tz), aendelea kuthibitisha kipaji chake kwa kuachia wimbo wenye hisia na ubunifu wa hali ya juu – SILENCE - sasa upo kwenye majukwaa yote ya kidigitali.’

Historia mpya imeandikwa rasmi katika muziki wa Tanzania pale jina la Meshack Fukuta, anayefahamika zaidi kama Meshamazing @amazing__tz, lilipotajwa mshindi wa mashindano makubwa ya kusaka vipaji vya kuimba nchini – Bongo Star Search (BSS) Msimu wa 10. Ushindi huu haukuwa tu furaha ya muda mfupi, bali umekuwa kumbukumbu isiyofutika kwa mashabiki wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Meshack Fukuta ni sauti mpya ya kizazi cha muziki bora, akitoa funzo kwamba muziki ni sanaa ya maisha, na mara tu unapouelewa, unakuwa sehemu ya nafsi yako. Kupitia kazi zake, amebadilisha namna ambavyo muziki wa Tanzania unavyotazamwa na kuthaminiwa, akituma ujumbe thabiti kuwa vipaji vya ndani ya nchi vina nafasi ya kung’ara kimataifa.

Leo, msanii huyu anazidi kuthibitisha ukubwa wa kipaji chake kupitia wimbo wake mpya “Silence”, ambao kwa sasa unapatikana kwenye majukwaa yote ya kidigitali ya kusikiliza na kupakua muziki. Wimbo huu ni zao la ubunifu wa hali ya juu na unatoa nafasi kwa mashabiki kujikuta wakitafakari maana ya upendo, maisha na muziki wenyewe.

Kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Tanzania nzima, huu ndio wakati wa kusherehekea mafanikio ya kijana huyu. Tunatoa mwito kwa wadau wa muziki, redio, televisheni, na mashabiki wote kumsaidia @amazing__tz kupaza sauti yake zaidi – kwa kusikiliza, kushirikisha na kuunga mkono kazi zake.
Mafanikio ya Meshack Fukuta ni ushindi wa muziki wa Tanzania, ni ishara kwamba vipaji vipya vinapewa nafasi na vinaweza kufika mbali. Ni wakati wa kuondoa ukimya – na kusherehekea “Silence.”

Credits to Yobex Fm 91.3

#BSSSeason10 #Silence #AmazingTZ #YobexFM91.3 #YobexEntertainment #LiveAndLoud#TmotionEntertainment

0 comments:

Post a Comment