Mbeya, Septemba 6, 2025 – Mashabiki wa soka na wadau wa burudani jijini Mbeya walishuhudia tukio lisilosahaulika wakati msanii nyota wa muziki kutoka mkoani humo, Zax (@zax_4real2020), alipotoa burudani ya aina yake katika sherehe za Mbeya City Day 2025.
Zax, ambaye ni miongoni mwa wasanii wakubwa waliotokea Nyanda za Juu Kusini, aliwasha moto jukwaani na kuwaacha mashabiki wa @officialmbeyacityfc wakicheza na kuimba pamoja naye kwa furaha kubwa.Akizungumza baada ya onyesho hilo, Zax alieleza kuwa siku hiyo imekuwa ya kihistoria kwenye safari yake ya muziki:
“mbeyacityfc imeniambia mimi ni mkubwa. Mashabiki wangu wamenionesha kuwa wanatamani kuniona kwenye matamasha makubwa kama haya,” alisema kwa furaha.
SIRI YA KUFANIKIWA
Zax alifunguka pia kuhusu siri ya yeye kuaminiwa na kupanda tena jukwaani katika tukio hili kubwa:
“Najivunia kuzaliwa Mbeya, naipenda timu yangu ya Mbeya City. Pia nipo active kwenye muziki – hii ndiyo siri ya mimi kuendelea kuaminika,” alisisitiza.
Ushirikiano wake na klabu ya Mbeya City FC umejidhihirisha si mara ya kwanza. Mnamo mwaka 2017, Zax pia alipata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha kubwa la Mbeya City Day, na hivyo kufanya 2025 kuwa mara ya pili kwa msanii huyo kuunganishwa na tukio hili muhimu.
HISTORIA INAYOENDELEA KUANDIKWA
Kwa Zax, burudani aliyotoa mwaka huu siyo tu kuwatumbuiza mashabiki, bali ni kuimarisha uhusiano wa muziki na michezo, na zaidi kuipa heshima Mbeya kama kitovu cha burudani na soka nchini.
Mahojiano yake maalum yalifanyika kupitia kipindi cha Hotshow cha @highlandsfm_tanzania, akizungumza na @mr_tee_kilaka_mashinee, ambapo alisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuipa Mbeya heshima kupitia sanaa yake.
#HighlandsFM
#MbeyaCityDay2025
#SisinawewePamoja
#ZaxTheGiant
0 comments:
Post a Comment