Baada ya golikipa wa Yanga, Metacha Mnata kufungwa goli la faulo lililozua gumzo kubwa kutoka kwa Allan Okello dhidi ya Yanga siku ya Ijumaa (22/05/2026), mjadala mkubwa umeendelea kuhusu namna ya upangaji wa ukuta kwa makipa wakati wa faulo.
- Wadau wengi wa soka walimlaumu Metacha kwa uzembe huo, hali iliyosababisha hata benchi la ufundi kumtoa nje mara baada ya tukio hilo.
Miongoni mwa waliotoa maoni yao ni Jemedari Said Kazumari aliyesema:“GK ambaye ni National Team Material unapangaje ukuta namna hii halafu unajificha nyuma yake?... Hili ni goli lake.”
Kabla ya tukio hilo, Ngome ya Michezo ilifanya mahojiano maalum na golikipa wa zamani na kocha wa makipa — Aswile Asukile, ambaye alifafanua kwa kina namna sahihi ya:
- Kupanga ukuta
- Kusimama wakati wa faulo
- Kusoma angle ya mpira
Somo ambalo wengi wanaamini lingeweza kumsaidia Metacha kuepuka kosa lile.
Full Interview ya Aswile ipo hapa https://www.youtube.com/watch?v=-hdFxpoAUK0
Tazama sasa!
#Metacha #AswileAsukile #NgomeYaMichezo #Yanga #SokaLaBongo







0 comments:
Post a Comment