skip to main |
skip to sidebar
HILI NI JANGA
HII RIPOTI IMENISIKITISHA SANA
Wasichana wa Nzovwe jijini Mbeya wanapenda kupigwa 'mtungo'
WASICHANA wa eneo la Nzovwe, jijini Mbeya wametuhumiwa kushinda katika
klabu za kuuza pombe za kienyeji, hasa nyakati za usiku na kufanya
mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja kwa siku kwa tamaa ya fedha.
Imedaiwa tabia ya wasichana hao, kupenda kuomba fedha kwa wanaume
tofauti wanaokuwa wanakunywa pombe katika klabu hizo, hupelekea mwisho
wa siku wakubali kufanya ngono zembe na mwanaume zaidi ya mmoja.
Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na wakazi wa eneo hilo, katika
mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Vijana Mabalozi Watanzania wanaoishi
na virusi vinavyosababisha Ukimwi (TAYOPA).
Mkoa wa Mbeya ni wa
nne kutembelewa na TAYOPA ambao wapo kuutambulisha mradi wao uitwao
'Vijana Tuzinduke ili kujikinga na Ukimwi'.
Mikoa mingine iliyotembelwa ni Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na baadaye wataelekea Ruvuma.
Mradi huo unafadhiriwa kwa pamoja na na shirika la Afya la Kimataifa
(FHL) na kituo cha televisheni cha MTV cha nchini Marekani.
Wakizungumza wakazi hao wa Nzovwe walisema kuwa wasichana wa kike wa
maeneo hayo, wamekuwa wanaendekeza sana kuombas fedha kwa wanaume katika
klabu za pombe nyakati za usiku hali inayopelekea kuwepo kwa ngono
zembe na wanaume wengi kwa siku.
Mkazi aliyejitambulisha kwa
jina moja la Joyce alisema hali hiyo imefanya wasichana hao ambao bado
ni wanafunzi wa shule za msingi, kupenda kufanya ngono na wanaume wengi
mtindo ambao ni maarufu zaidi kwa jina la 'Mtungo'.
"Huku
unaweza kumuona msichana ukadhani ni mdogo, kumbe anao uwezo wa kufanya
mapenzi na zaidi ya mwanaume mmoja kwa siku...kimsingi hali inatisha
kwani huwa wanafanya ngono zembe".Joyce alisema
Naye Mwenyekiti
wa TAYOPA, John Solanya, alisema yeye alipimwa afya na kugundulika kuwa
na maambukizi ya virusi vya Ukimwi tangu mwaka 1995, ambapo
alijitangaza.
Solanya alisema kuwa anaishi na mke pamoja na
mtoto mmoja ambao hawajaambukizwa Ukimwi, na kuwa tangu mwaka huu
hajawahi kuumwa hadi kufikia hatua ya kulazwa hospitalini kwani amekuwa
anazingatia ushauri anaopewa.
"Nina mke na mtoto ambao wao hana
maambukizi ya Ukimwi... ninapotaka 'chakula cha usiku' kutoka kwa mke
wangu huwa tunatumia kondomu" alisema Solanya.
Naye Fitina
Mohamed, ambaye pia anaishi na virusi vya Ukimwi, alisema ni wengi
wanayo maambukizi ya ugonjwa huo lakini huwezi kuwatambua kwa
kuwaangalia kwa macho bali hadi wapime na kujitangaza.
Alihoji
kuwa ni nani ambaye angeweza kuwatambua kuwa yeye ama mwenzake Solanya
wanaishi na virusi vya Ukimwi iwapo wangeamua kukaa kimya mara baada ya
kupima afya zao, na kuendelea kukubali kufanya ngono zembe.
Tukio hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii Fareed Kubanda 'Fid
Q. na mshindi wa Bongo Star Search, Jumanne Idd ambao waliweza kutoa
burudani kabambe na kuwa kifutio kikubwa katika mkutano huo.
NZOVWE
ndo sehemu niliyokulia naweza kuwa shuhuda wa mambo jinsi yanavyokwenda
ila sikuwahi kufikiria kama hali inaweza kufika hapo ilipofika
sasa.BLOGGER wa Blog hii nina maslahi binafsi na Nzovwe so siwezi kukaa
kimya kutokana na ripoti ya huu utafiti.Lazima hatua za haraka zifanyike
ili kuokoa kizazi cha sasa na kijacho.
Stori hii ilitoka mwezi wa kumi na mbili source-www.jamiiforums.com nimeamua kuirudia ili kutafuta njia za kuokoa jamii maana mimi naona hili ni JANGA
0 comments:
Post a Comment