Tuesday 9 April 2013

SIR ALEX AZUNGUMZIA GEMU YA JANA

Sir Alex Ferguson amedai Manchester United walikosa ‘bahati’ kwa kufungwa 2-1 na Manchester City hapo jana na pia alikiri kuwa, Siku zote, Timu yake ‘hujibebesha zigo’ badala ya kurahisisha kazi.
Ingawa jana walifungwa, Man United bado wapo kileleni wakiwa Pointi 12 mbele ya Man City na Mechi zikiwa zimebaki 7.
Kwa hali ilivyo sasa, Man United wanahitaji kushinda Mechi 3 na Sare 1 kati ya hizo Mechi zao 7 ili watwae Ubingwa ikiwa Man City watashinda Mechi za mbele yao.








































Akiongelea Mechi hiyo ya jana, Ferguson alidokeza Bao la kwanza la Man City lililofungwa na James Milner lilikuwa na ukiukwaji kwani kulikuwa na Ofsaidi.
Ferguson alieleza: “Tevez alikuwa akiingilia mchezo na alikuwa Ofsaidi. Alikuwa akimziba Kipa na kama hiyo si kuingilia mchezo, sasa sijui ni nini!”
Ferguson pia alipuuzia pale alipoambiwa kuwa kuongoza kwa Pointi 15 kuliwafanya Man United wabweteke na kucheza kichovu katika Mechi ya jana hasa Mkongwe Ryan Giggs ambae ndie alipoteza Mpira uliozaa Bao la kwanza.
Akipuuza dhana hiyo, Sir Alex Ferguson amesema mkazo wao sasa ni kushinda Mechi ijayo watakayocheza ugenini Jumapili na Stoke City na Siku 3 baadae wapo tena ugenini huko Upton Park kucheza na West Ham na kufuatia Mechi ya Nyumbani Old Trafford dhidi ya Aston Villa.
Alisema: “Hatutabweteka. Ukiangalia Historia ya Klabu hii, kwa Miaka mingi tumekuwa tukijipa ugumu wenyewe na kuwaacha Mashabiki wetu roho mkononi! Lakini tunaongoza kwa Pointi 12 na bado zipo Mechi 7 tu. Kila gemu tunayocheza, unapunguza Mechi. Mkazo wetu sasa ni Stoke hapo Jumapili.”







































































0 comments:

Post a Comment