Kila mafanikio yana hadithi yake, na kwa upande wa Stand Up Comedy Mbeya, jina moja limesimama imara kama msukumo wa maendeleo na ubunifu — Inno Presenter, kwa sasa anafahamika pia kama The Events Doctor (Sisi Burudani Mbeya tumembatiza jina hili)
INNO PRESENTER ni zaidi ya jina la kawaida kwenye tasnia ya burudani mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla. Ni kiongozi mwenye maono makubwa, mwepesi wa kubuni na kutekeleza mikakati, na mbunifu wa matukio ambaye amekuwa sehemu muhimu ya ukuaji wa Stand Up Comedy Mbeya, jukwaa linaloongozwa na Mbeya Boy.
Safari yake ya kipekee ilianzia kwenye
mawimbi ya hewa ya redio ACCESS FM
ya Mbeya, ambako alijulikana kama mtayarishaji, mzalishaji, mtangazaji na
mbunifu wa vipindi vya burudani — akiweka alama kupitia kipindi maarufu cha HOME BASE. Sauti yake ya kipekee na
maudhui yenye mvuto vilimfungulia milango ya mafanikio zaidi kwenye sekta ya
burudani na media.
Mbali na uhodari wake kwenye redio, Inno Presenter amejiimarisha katika ulimwengu wa kidigitali kupitia TALK WITH INNO PODCAST, jukwaa la sauti linalowapa watu nafasi ya kusikiliza mazungumzo yenye maarifa, burudani, na motisha kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya tasnia.
Kama Creative
and Promotion Manager wa Stand Up
Comedy Mbeya, amekuwa kiungo muhimu kati ya wasanii, mashabiki na waandaaji wa
matukio. Kupitia uwezo wake wa kupanga na kutekeleza promosheni zenye mvuto,
matukio kama vile Easter Comedy Show yamepata umaarufu mkubwa na kuonesha
ukuaji wa kweli wa sanaa ya vichekesho mkoani Mbeya.
Imedhihirika na kuthibitika kwamba, Inno Presenter ni zaidi ya mtu wa matukio — ni daraja linalounganisha vipaji na fursa, mtu wa suluhisho na msukumo wa mabadiliko chanya kwenye tasnia ya burudani. Juhudi zake, nidhamu yake na mapenzi yake kwa sanaa vimeweka msingi imara wa mafanikio ya jukwaa la Stand Up Comedy Mbeya.
Imeandaliwa na KIZZ1
Email: burudanimbeya@gmail.com
Instagram @burudanimbeya
Youtube: Burudani Mbeya
Blog: https://www.burudanimbeya.blogspot.com
Allrights reserved @BURUDANI MBEYA MEDIA
💪
ReplyDelete