Thursday 2 May 2013

BREAKING NEWS: FIFA YAWARUDISHA WAMBURA NA MALINZI

Malinzi, Wambura warudishwa kugombea TFF na FIFA.


Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
 
 
Kuna taarifa kwamba wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 
Taarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo imeshatua Fifa tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa wanagombea. 
Uongozi wa TFF unatarajia kuzungumza nusu saa ijayo kuanzia sasa katika ofisi zake katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam. 
Taarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo imeshatua TFF tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa wanagombea.
 Endelea kufuatilia kufuatilia safu hii kwa habari zaidi.

0 comments:

Post a Comment