Friday 5 April 2013

Ray aachana na filamu yake ya Sister Marry

RAY ASALIMU AMRI BAADA YA KUKUBALI KUACHANA NA
FILAMU YAKE ILIYODAIWA KUWA INA UDHALILISHAJI
MKUBWA

HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’,
Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa
kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji
huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.

Cover la filamu ya Sister Marry.


Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama
Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile
kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa
namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Ray amebainisha kuwa
baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye
filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata
akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati
mwingine.

“Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo
walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa
nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda
nije kuirudia upya hapo baadaye,”
Alisema Ray


Source JF

0 comments:

Post a Comment