Friday, 5 April 2013

EXCLUSIVE Interview na Watukufu Camp



MAMBO YALIKUWA HIVI
Blogger:grrrrr grrrrrr
Monky:hallow!
Blogger: Inakuaje jembe?
Monky:poa,nani anaongea?
Blogger:Najitambulisha
Monky:ha ha haaa….inakuaje big?
Blogger:Aisee sio mbaya,vipi michakato inasemaje?
Monky:Mungu anasaidia sio mibaya,aisee big kitambo sana ujue!
Blogger:Kweli kitambo kwanza hongera nimembiwa unafamilia saivi
Monky:asante big si unajua tena
Blogger:Ok,hebu niambie nini kinaendelea WATUKUFU Camp?
Monky:Watukufu Camp inaendelea vizuri sana naweza kusema ni kundi pekee linalofanya vizuri sana tangu kipindi hicho mpaka saivi.
Blogger:Whatt????????
Monky:YES.
Blogger:Hebu jaribu kueleweka brother.
Monky:Nimeeleweka vizuri brother sema hujanielewa  ‘Watukufu tupo/wapo hata sasa hivi nikikwambia nitajie wasanii watatu wanaokimbiza gemu ya Mbeya lazima msanii kutoka Watukufu camp litakuwepo’.
Blogger:Mh! Tuna vitu vingi vya kuongea na wewe brother maana mi sijaelewa.
Monky:bro unanichokonoa niseme vitu ambavyo sikuwa tayari kuvisema ila kwa kifupi ni kwamba kundi lipo ila wasanii wapo bize na solo project zao na wanafanya vizuri sana tu
Blogger:Kwanini solo project?
Monky:Kama unavyojua kundi hili lilianzishwa mwanzo mwa miaka ya 2000 tukiwa zaidi ya wasanii kumi na wote tulikuwa ni wanafunzi wa sekondari na msingi,kilichotokia ni kutokana na masuala ya kielimu tukaanza kutawanyika taratibu kwa mfano DrFazi alikwenda kusoma Uganda,DrCruel na Ezekia walikuwa bize na masomo ya form five na six,WaveB ,BaveD na mimi mwenyewe pia tulikuwa bize na shule vivyo hivyo na wasanii wengine.
Blogger:Nini kilifuata?
Monky:Baada ya hapo harakati za shule zikaendelea saivi ninavyoongea na wewe kuna watu wana digrii zao mkononi na wengine wanafanya masters.
Blogger:Unaweza nitajie wasanii walikuwa wanaunda kundi hilo baadhi?
Monky:Kiongozi wa kundi alikuwa ni Emmanuel Sanga(drcruel) anayefanya Masters pale kwenye chuo cha ST.Augustine Mwanza,member wengine ni drFazi mtwale na Ezekia ambao wanafanya vizuri kabisa kwenye muziki baada ya kupata digrii zao TEKU na IFM pia hawa jamaa ni waajiriwa .Drfazi anafanya vizuri upande wa muziki wa kizazi kipya na Ezekia anafanya vizuri upande wa muziki wa injili.Pia Raymond mkali wa freestyle Tanzania kapita hapa vipi niendelee broo?
Note:WATUKUFU CAMP ni kundi la muziki wa kizazi kipya lililoanzishwa mwanzoni kabisa mwa miaka ya 2000 na makao yao makuu yapo Nzovwe Mbeya mjini lilitamba na kibao chao kilichosumbua sana kipindi hicho kilichokwenda kwa jina la WANADATA NA MIMI  wakimshirikisha mkali wa RnB Qjay,kundi hili lilikuwa likiundwa na Drcruel-kiongozi,Drfazi,EzyG,Dobochizi,Monky,WaveB(Tozy),BaveD,Mjomba na wengine wengi.
Blogger:Ngoja tufanye kuwatafuta memba wengine maana kuna vitu vingi sana jamii inataka kujua toka kwenu.
ENDELEA kutembelea blog hii ili kupata undani kamili mahojiano haya kuna vitu vingi nimevipta ambavyo wengi hawavijui kuhusiana na kundi hili.
utapata kujua yafuatayo:
Je kweli hili kundi lipo?
Kama lipo wanafanya nini?
Memba wengine wanasemaje?
Nini tutegemee kutoka kwao?
Suala la mapenzi linahusika vipi kwa kinachoendelea katika hili kundi?
Picha za wasanii wanaounda/waliounda kundi hili utazipata hapa hapa
Na mengine mengiii……….


0 comments:

Post a Comment