Akizungumza jijini Dar es Salaam hili hivi karibuni Gadna alisema kuwa ‘tweets’ alizoziweka msanii huyo zinalenga kufikisha ujumbe alioukusudia hususani kwa baadhi ya watu wanaomuwekea mipango mibaya ya kuharibu kazi zake za kimuziki
Alisema kuwa wapo baadhi ya washika dau wanaojikita katika maswala ya muziki kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wakimnyonya mwanamuziki bila ya kujali jasho lake na nguvu yake kwa kazi anayoifanya
Kutokana na hali ya kunyonywa wasanii na washika dau hao alisema msanii atakapopata akili na kuwa na uwezo wa kugundua kuwa ananyonya na hawezi kufika mbali hali inabadilika kwa kuanza kukandamizwa na kuwekewa vikwazo katika kazi zao
“Baadhi ya washika dau wanawaogopa wasanii wakubwa kwa kuwa tishio katika biashara zao hivyo hata wasanii wachanga pia wananyimwa nafasi ya kukua kisanii kwa kuhofia kuja kuwageuka baadaye pindi watakapopata nafasi ya kufanya hilo” alisema Gadna
Aliongezea kuwa mfumo wa muziki hauko sawa na upo kwa lengo la kumnyonya msanii hali ambayo inazidi kudidimiza wasanii na muziki wa nchi hii hali inayosababisha muziki unakuwa kwa kusikilizwa redioni na si kwa kukuwa kwa kipato kwa wasanii
Alisema kuna hujuma zinazoendelea kwenye soko la muziki zenye lengo la kumnyonya mwanamuziki na kumpa utajili mdau wa muziki sababu hiyo inapelekeea wanamuziki wa nchi yetu kutoendelea katika soko la muziki
Lady JayDee hivi karibuni amekuwa akitumia mtandao wa Twitter kwa ajili ya kutuma ’tweets’ zenye ujumbe kwa mtu aliyemkusudia ingawa hazikuonyesha wazi wala kutaja jina la muhusika.
SUGU a.k.a Mr2 ambaye kwa sasa ni mbunge wa kuchaguliwa wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwakilisha jimbo la Mbeya Mjini ambaye anachukuliwa kama MFALME na MUASISI wa muziki wa kizazi kipya Tanzania na Afrika mashariki ndiye alikuwa wa kwanza kabisa kulalamikia hili suala la mfumo wa unyonyaji wa muziki Tanzania na wanaouendesha huo mfumo aliwataja waziwazi kwenye vyombo vya habari,mtaani,Bungeni na hata kwenye kitabu chake kinachoitwa 'From Street to the Parliament'.
Lady JayDee
Sasa kama kama Mfalme mheshimiwa SUGU aliongea halafu MALKIA Judith Wambura a.k.a lady JayDEE naye anaongea suala hilohilo hapo sidhani kama mtu hata kama haujui kusoma je hata picha hauioni?Mfumo huo ni lazima ufumuliwe na wa kuufumua ni nani?
Mh.SUGU siku aliyokuwa akila kiapo Bungeni Dodoma
0 comments:
Post a Comment