Wednesday 4 December 2013

ROMA ASISITIZA PESA NDIO ILIMALIZA VITA YA RUGE na SUGU

SUGU na RUGE wakiwa na Nchimbi na mwanasheria LISSU
ROMA kubitia website ya amesisitiza kuwa ni kweli kabisa pesa ndiyo iliyomaliza vita ya RUGE na SUGU,na hiki ndicho alichokisema;
'Hapa sasa "pesa ilimaliza vita ya ruge na sugu"!! -shortly ni kuwa issue ya brother sugu kuingia katika vita hii kama ilivyosemwa awali na ilivyoonekana POINT ilikuwa kuitetea sanaa, ambayo ni wasanii pia wakiwemo ndani hapo...kuwa wanachokipata hakistahili kulinganisha na kazi wanayofanya!! malipo mabovu ya show, uuzwaji mbovu wa kazi za sanaa unawafaidisha wengine kuliko wasanii,na mengine mengi sana tuliyasikia!! ambayo kimsingi yote yanaegemea kwenye kipato = pesa!! Lakini baadae ikaja semwa na pande zote mbili zikakiri kuwa songombingo hilo limeisha baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa yote yaliyokuwa yakilalamikiwa yameeleweka na upande wa brother ruge umekubali kuyamaliza yote yaliyokuwa yakilalamikiwa kuwa sasa yameisha na yanatekelezwa!! Sasa hiyo ina imply nini? kama yameisha ina maana tatizo la malipo duni ya wasanii, tatizo la wasanii kuingiza pesa nyingi na kulipwa kidogo tofauti na wanachoingiza..na yote yaliyoongelewa' .
 SASA YAMEFIKIA KIKOMO!!! BASI NI HABARI NJEMA KWA WASANII.... na hiyo yote ni nini? - ni kuwa sasa watapata kipato sawa na haki yao!! -wataifanya sanaa yao kwa njia sahihi na za faida kama ilivyokuwa ikihitajika ktk vita hiyo!! -na wataiona faida ya sanaa kwa ujumla!! KIPATO=MALIPO=PESA BASI PESA NDO IMAMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU!! 2030 YA R.O.M.A NAYAJIBU NINAYOULIZWA NA YANAYOHITAJI UFAFANUZI!!!

0 comments:

Post a Comment