Chuo kipo chini ya kampuni ya Radio Consult Limited na makao
makuu yake ni Mbeya maeneo ya nanenane jengo la Chai.
Kwanini Digital Media College of Tanzania?
Kwasasa kuna vyuo vingi sana hapa nchini vinavyofundisha
kozi hizi za media ukiwemo uandishi wa habari na utangazaji, changamoto kubwa
iliyojitokeza ni kwamba wahitimu wote wanaomaliza katika vyuo mbalimbali wengi
wao wanakosa ajira na kibaya zaidi wanashindwa kutumia elimu yao waliyoipata
hata kujiajiri kwa kuandika habari, kumiliki mitandao (websites), kuandika na
kuhariri vitabu, kutafuta fursa mbalimbali kwenye mitandao, kujiunga katika
vyama mbalimbali ulimwenguni vinavyojihusisha na masuala ya uandishi wa habari,
kuandaa makala na kushiriki kwenye mashindao mbalimbali. Kuna mambo mengi sana
ambayo mwandishi wa habari anaweza kuyafanya bila kuajiriwa yaani namaanisha
kwa kujiajiri mwenywe.
Hii ndiyo sababu kuu ambayo chuo cetu cha DMCT kinapenda
kuiangalia kwamba kwa mwandishi wa habari yeyote yule kuanzia ngazi ya chini
kabisa hadi ya juu wawe na uwezo wa kujiajiri wenyewe. Kuna tofauti kubwa kati
ya nchi yetu na nchi za Africa Mashariki na Ulaya kwamba sisi mwandishi wa
habari hutegemea ajira tu katika chombo cha habari na akikosa hpo anarudi
kulala nyumbani na kulal mika hakuna ajira.
Katika kutafakari ni kwa njia zipi tutazitumia kumsaidia
mwanafunzi au mwandishi wa habari aweze kujiajiri hata pale anapokosa chombo
cha habari cha kufanyia kazi, DMCT tumeona ni bora tufundishe kozi zifuatazo
kwa mwaka 2014:-
Certificate in digital Journalism kwa mwaka 1. Na
Certificate in Radio Production kwa mwaka 1.
Hii kozi ya digital journalism itawawezesha wanafunzi wote
kuanza kutengeneza pesa hata kama ni kiasi kidogo wakiwa wanasoma kutokana na
kazi za vitendo watakavyokuwa wanazifanya, kama kuandika habari na makala na
kuziuza katika mitandao mbalimbali nje na ndani ya nchi. Pia watafundishwa
masuala ya kumiliki mitandao (website na blog) kwa undani zaidi hali
itakayowawezesha pia kuendelea kujipatia pesa. Vile vile kozi ya uandaaji wa
vipindi ambayo itatoa waandaji wa vipindi wenye ujuzi wa hali ya juu ambao
wanaweza hata kuuza vipindi vyao kwenye vyombo vya habari mbalimbali.
Details za chuo.
Uwezo wa kupokea wanafunzi: 50 tu kwa mwaka 2014.
Kozi: Certificate
in digital Journalism
Certificate in
radio production.
Muda: Mwaka mmoja
kila kozi atleast miezi 12 hadi 14. (miezi 2 ni English and computer course
advanced course kuhakikisha kila mmoja anaweza kuongea English bila shida
lakini pia anaweza kutumia computer bila shida, maana fursa nyingi zipo kwenye
kiingereza na zinamtaka mtu awe na uzwezo wa kutumia computer) Miezi mingine 3
ni field na miezi iliyobaki ni masomo ya darasani na vitendo.
Uwiano wa mafunzo kwa
vitendo: Chuo kinataraji kutumia mpaka 70% ya mafunzo kwa vitendo na 30%
mafunzo ya nadharia.
Field tour:
Tunatarajia kufanya filed tour mbalimbali kama
ifuatavyo:-
Field tour kutembelea chombo cha habari cha nje.Pia kutakuwa na tour mbalimbali kama kutembelea wakulima
waliofanikiwa, kutembelea vyombo vya habari mbalimbali katika mikoa mbalimbali.
Mazingira ya
kujifunzi: DMCT ina mazingira mazuri kwani mpaka sasa maandalizi
yamekamilika Darasa la computer litakuwa na computer 20, pamoja na studio ya
kisasa ya kujifunzia ambayo pia itatumika kwa kazi za kurekodi kwaya na mziki.
Walimu mbalimbali wenye uzoefu watakuja kufundisha.
Ada: Kwa mwaka ni
Tshs 600,000/= Laki sita tu au Dola 600 kwa wanafunzi kutoka nje. Malazi na
chakula watajitegemea, lakini chuo kimewatafutia hostel kwa wanafunzi watakao
taka kukaaa hostel.
Simu: 0718 114932 au 0763 099842 au 0686235888,
P
o Box 2213 Mbeya.
Tunapatikana
Nanenane Jengo la Chai RSTGA!
Kozi zingine tunazotarajia kuongeza baadaye ni:- Music
Production, TV Production, ICT.
0 comments:
Post a Comment