Thursday, 26 October 2023

T-MOTION ILIBAHATIKA NA AMMY CHIBA

Kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa LEBO ya T-Motion Entertainment wameandika haya:
Ammychiba ndiye msanii bora wa kike wa muda wote kabisa kuwahi kutokea nyanda za juu kusini ambaye anaheshimika na kukubalika na kila mtu ambao ameupata kwa uwezo wake unaotokana na ubora wa kipaji chake cha hali ya juu kabisa.
Ilikuwa ni BAHATI kubwa kwa taasisi yetu kufanya na Ammychiba. Kipindi tunaanza kufanya naye kazi Ammychiba alikuwa ndiye msanii mkubwa kabisa nyanda za juu kusini so kwetu ilikuwa ni BAHATI sana kufanya naye kazi ikizingatiwa sisi ndio kwanza tunaanza halafu lakini yeye akatuamini so kwetu ilikuwa ni BAHATI. 

Kufanya kazi na Ammychiba kulileta faida nyingi sana kwetu:-
1) Kulisababisha tufuatiliwe kwa ukaribu sana na mnyororo mzima unaoizunguka tasnia ya muziki kwasababu a) Ammychiba alikuwa amekaa kimya kwa muda kiasi kwenye muziki so wadau walitaka kujua atarudi vipi b) walitaka kujua hii 'lebo' ndogo mpya inayofanya kazi na Ammychiba ina kitu gani maalum mpaka Ammychiba kakubali kufanya nao kazi.
2) Kufanya kazi na Ammychiba kulifanya tuaminike,IMANI aliyotupa Ammychiba kulifanya tasnia pia ituamini maana yeye alikuwa anaaminika na tasnia na kitendo cha yeye kutuamini automatic na tasnia ikatuamini.

Itaendelea...

#MajorMega2023
https://www.instagram.com/reel/Cy23CV4to1V/?igshid=NjZiM2M3MzIxNA==

1 comments: