skip to main |
skip to sidebar
TAKUKURU yawasafisha wachezaji Azam
TAKUKURU YAWASAFISHA WACHEZAJI WA AZAM
AMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
S. L.P. 42325,
Temeke,
Simu: 022 2850633,
Nukushi: (022) 2850635,
Baruapepe:rbctemeke@pccb.go.tz,
Mtandao www.pccb.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UCHUNGUZI WA WACHEZAJI WA TFF
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa taarifa kwa
umma kwamba, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Temeke dhidi ya
wachezaji wanne wa timu ya soka ya AZAM waliokuwa wakituhumiwa kupokea
hongo/rushwa ili kupanga matokeo, haukuweza kuthibitisha tuhuma hiyo.
Kosa la kupokea rushwa ni kinyume na Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa
kifungu hicho ni kosa kwa mtu yoyote kuomba, kupokea, kushawishi au
kulazamisha kupewa rushwa au kuahidi kutoa rushwa.
Wachezaji
waliokuwa wakilalamikiwa ni (1) DEOGRATIUS BONIVENTURE MUSHI (DIDA), (2)
ERASTO NYONI, (3) SAID HUSSEIN MORAD na (4) AGGREY MORRIS. Wachezaji
hawa kwa pamoja walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo
ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SPORTS CLUB iliyochezwa tarehe
27/10/2012 katika Uwanja wa Taifa – jijini Dar es salaam. Katika mechi
hiyo AZAM FC ilifungwa magoli 3 - 1.
Tuhuma hizo ziliwasilishwa
TAKUKURU Mkoa wa Temeke tarehe 9/11/2012 kutoka AZAM FC ikiwatuhumu
wachezaji hao kupokea kiasi cha shilingi milioni saba (7,000,000/=)
kutoka kwa uongozi wa Simba Sports Club ili wagawane na kupanga matokeo
ya mechi. Fedha hizo zilidaiwa kupokelewa siku moja kabla ya mechi kati
ya AZAM FC na SIMBA SC (tarehe 26/10/2012).
AZAM FC, imeweza
kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa
kwa kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU – chombo ambacho
ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kisheria kuchunguza makosa ya
rushwa.
Tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wananchi kwa
ujumla, kuendelea kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU ili kwa
pamoja tuweze kudhibiti vitendo vya raushwa katika nchi yetu
Imetolewa na Doreen J. Kapwani - Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Jumatatu tarehe 08/04/2013
0 comments:
Post a Comment