KIUNGO
mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Madaraka Selamani,timu za
Chile na Mexico,zili staili kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka
huu kutokana na kiwango walichoonesha.
Madaraka aliyewahi kuichezea klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa
ikiwemo kuibebesha ubingwa wa Tanzania bara mara tatu,alizitaka timu za
Afrika kuiga mfano wa timu hizo kutokana ushindani waliouonyesha licha
ya kutolewa katika hatua ya mtoano.
“Timu za Afrika zinapaswa kuiga mfano wa timu za Chile na
Mexico,ambazo hazikuwa na wachezaji wenye majina makubwa lakini
zilionyesha ushindani wa kweli na kuwatoa jasho waandaji wa fainali hizo
Brazili,”alisema Madaraka.
Mkongwe huyo pia alisema haipi nafasi Brazili ya kunyakua ubingwa huo
kwa sababu imeonyesha kuwa na mapungufu mengi licha ya kufika hatua
hiyo ya robo fainali.
“Hii siyo Brazili ile ambayo tulikuwa tunaifahamu ambayo huiwezi
kumaliza dakika 90, pasipo kutikisa nyavu za wapinzani tumeshuhudia
mechi mbili ile ya
Mexico na Chile,ikimaliza bila ushindi siyo jambo
zuri kwa sababu penalty ni bahati,”alisema Madaraka.
Madaraka alisema kocha Luis Fillipe Scolar,ameshindwa kufanya
uchaguzi mzuri wa wachezaji kama alivyofanya mwaka 2002,wakati
alipochukua ubingwa wa dunia kwa mara ya tano Korea Kusini na Japani.
“2002 alifanya uteuzi wa wachezaji sahihi na kupata timu ambayo
ilikuwa ikiogopewa lakini inaonyesha mwaka huu amechemka hata ushindi
wao ni kama wa kubahatisha na mbaya zaidi wapo nyumbani Scolari anapaswa
kuwa makini,”alisema Madaraka.
Mkongwe huyo alimalizia kwa kuisifia timu ya Uholanzi ambayo imekuwa
ikifanya vizuri tangu kuanza kwa michuano hiyo na kusema kama itaendelea
hivyo inaweza kufuta machungu ya mwaka 2010 na kutwaa taji hilo.
Source:goal.com
Sunday, 6 July 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment