Tuesday, 3 April 2018

MESHAMAZING - Nitulize





Karibu uitazame video mpya kabisa ya Mwanamuziki MESHAMAZING inayokwenda kwa jina la NITULIZE ambaye ni mshindi wa Super Nyota 2017 kama ilivyoongozwa na Director Steve Ombella na Audio imefanywa na mtayarishaji J-Wilz kutoka studio za E-records. mesha anasema hii ni video yake ya tatu lakini ni video yake ya kwanza rasmi na ndani ya mwaka huu ataachia video zaidi ya tatu ambazo zipo tayari zinangoja muda tu.



Msanii huyu kwa sasa ndiye msanii mkali kwa nyanda za juu kusini lakini pia ndiye msanii pekee nyanda za juu anayemiliki bidhaa zake ambazo ni AMAZING UBUYU NA AMAZING GROUND NUTS (KARANGA) ambazo amezizindua march 23,2018.

0 comments:

Post a Comment