Tuesday, 8 August 2017

A – Z YA LOVE,MELODIES & COVER NIGHT


Show iliyokuwa gumzo sana jijini kwa kipindi cha takribani wiki mbili hivi ilihitimishwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 4/8/2017 pale Club K-Mo zamani Kiwira Motel Soweto. Show hii ilijengwa kuwazunguka wasanii wa
tatu ambao ni Zax for Real anayetajwa kama msanii wa kiume mwenye mashabiki wengi Mbeya na nyanda za juu kusini kiujumla,Ammy Chiba anayetajwa kama Malkia wa nyanda za juu kusini na Meshamazing ‘COBRA’ anayetajwa kama msanii mkali- hatari sana anayechipukia nyanda za juu kusini lakini pia ni kipenzi cha Mbeya Movies. Pia show ilipambwa na wasanii wengine wakali kama Mtafya,Qairasar,Ken Eyes (akiwakilisha chunya),Chwaka Melody(Mbeya vijijini) na wengine wengi wakiwakilisha wilaya za Mkoa wa Mbeya,Songwe na Iringa. Show hii iliongozwa na Best Male Mc of all time wa Nyanda za juu kusini Prince Ramalove na Current female Mc wa Mbeya Saraphina Jerry ‘The Diamond Voice’ huku kwenye mashine alianza Dj Bura akapokewa na Rdj Speed halafu akamalizia DjFrank ‘fantastic’.

22:00 Walipanda Mc’s wa show Prince Ramalove na Saraphina kuifungua show na kuanza kuwapandisha wasanii kwa mtindo wa bampa to bampa au bandika bandua. Walianza kupandisha wasanii kutoka wilayani ambao walionyesha uwezo wa hali ya juu sana hali iliyowashangaza watu wengi mpaka saa sita kamili.
00:00 Mc’s akamkaribisha Mwakilishi kutoka Tmotion lakini katika hali ya kushangaza akapanda mdau wa muziki Eliud samwel ambaye aliongea kwa niaba ya kampuni lakini pia alitumia kunadi shughuri zake na kampuni.

00:07 Alipandishwa Rapa mtanashati Qaraisar aliyeshusha bonge la show lililojaa bonge la utulivu na ubunifu.
00:20 Hapo ndio balaa lilipozidi maana ukumbi ulilipuka kwa shangwe la ugweeeeee….hapo alipanda free style master Mtafya wa kutukuyu kusauzi,alipiga free style kwa muda wa dakika kama ishirini hivi halafu akamaliza na wimbo wake wa kutukuyu kusauzi huku mashabiki wakitaka aendelee na show akapotea jukwaa.

00:45 Balaa lilizidi alipanda mshikaji ambaye hapendi umuite msanii bali anataka aitwe True definition of Entertainer (Maana halisi ya mburudishaji ) anakwenda kwa jina la Neka beats pia ni producer kutoka studio za Tmotion music nzovwe. Jamaa alipiga show ya maana hadi mashabiki wakamrudisha jukwaani arudie tena na akarudia wimbo mmoja.
MESHAMAZING,AMMY CHIBA NA ZAX FOR REAL
Walianza show yao kuanzia saa saba kamili usiku,walipiga live flani hivi ya kipekee huku wakipeana tafu kwenye back vocal.

01:00 Alianza meshamazing aliyepiga show ya maana sana huku akipigiwa shangwe mwanzo mwisho ofcoz pia Mbeya movie star hawakumuangusha pia kwenye kumshangilia.
01:15 Akapanda ammy Chiba kipenzi cha wengi naye kama kawaida hajawahi kosea,alipiga show bab kubwa yenye viwango kama ilivyotarajiwa na wengi.
01:35 Akamaliza show Zax for real mwenyewe kwa kudondosha show heavy weight kwa namna ambayo hajawahi fanya,alitumia kama dakika ishirini tu lakini mashabiki waliridhika na walichokipata.
02:00 Ikawa ni muda wa kuoneshana upendo ambapo watu mbalimbali walilishwa keki,tukio hili liliongozwa na Boaz Chesco matandara wa Gfm kupitia kipindi chake cha love jam.

MASTAR

Tukio hili lilihudhuriwa na mastar kibao wa green city kutoka Nyanja mbalimbali kuanzia kwenye michezo (Raysir –Mbeya city fc),redio personalities(presenters,djs,managers,etc),movie stars ,Musicians,wadau wa muziki etc lakini katika wote alikuwa kivutio ni ndugu Chance Kashililika maarufu kama Kashili muuza mayai aliyejizolea umaarufu kupitia vichekesho vyake mtandaoni kama vile muuza mayai aliyefumaniwa,mjomba wa mwakyembe n.k

MAPUNGUFU
Mapungufu yalikuwepo ingawa hayakuwa makubwa sana,mfano show kuchelewa kuanza,vinywaji kutokuwepo vya kutosha,kuna wakati flani kidogo mawasiliano kati ya dj na msanii kutokuwa sawa.
TATHMINI
Tathmini yetu wana burudanimbeya ya show ni kwamba show hii ilifanikiwa kwa kiwango cha juu sana,ni show ya pili kufanikiwa baada ya ile ya Mask Party. Naweza kuipa alama 87%.
Tunatumia fursa hii kuwapongeza waandaji wa hii show kwa kuthubutu na kuweza kufanya kitu kizuri.

Kwa maoni/ushauri/habari n.k wasiliana nasi kupitia burudanimbeya@gmail.com


0 comments:

Post a Comment