Wednesday, 12 December 2018
Meshamazing - Sina Thamani (Official Video Hd)
Msanii wa muziki wa kizazi kipya jijini Mbeya ambaye pia ni mshindi wa Shindano la Super Nyota 2017 na Bongo Star search mbeya 2018 ameachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la SINA THAMANI.
Anasema video yake imeongozwa na CLINTON KUCCI wakati audio imefanywa na KELVIN wa T-MOTION MUSIC lebo anayotokea.
KUHUSU GHARAMA anasema 'video hii
haijatumia gharama ndogo sana wala kubwa sana kwasababu kuna mahitaji ambayo yalihitaji pesa tuliyapata bila pesa lakini pia kuna mahitaji mengine mengi tulitumia pesa lakini pia napenda kumshukuru muongozaji wa video hii Clinton Kucci kwa kufanya uwepesi kwenye kazi hii pia bila kumsahau Director Azalia kwa sapoti kubwa aliyoitoa kwenye kazi hii,namshukuru pia Vixen rafiki na dada yangu Matilda Itala kwa kazi nzuri aliyoifanya na wote waliofanikisha kwa namna moja ama nyingine'.
Shukrani za pekee ziende kwa menejimenti yangu 'T-MOTION ENTERTAINMENT' kwa kufanikisha jambo hili.
Nashukuru vyombo vya habari vyote kwa kuwa na mimi wakati wote bila kuchoka naomba musiniache maana safari ndio kwanza inaanza.
Mashabiki zangu siwezi kuwasahau kabisa kwasababu nyie ndio nguzo yangu kuu.
Nawaahidi kuwa views za youtube zikiipita video yangu ya NITULIZE naachia video nyingine.
Niwatakie heri ya msimu huu wa sikukuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment