MBARALI | 09 OKTOBA 2026
Timu ya Kijiji cha Uturo imeibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5–4 dhidi ya Mtamba FC, baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo wa marudiano wa mashindano ya Rufiji Basin Cup 2026, yanayofanyika kupitia Mradi wa NBS Usangu.
Mchezo huo ulipigwa Ijumaa, Oktoba 9, 2026, kuanzia saa 10:30 jioni hadi saa 12:15 jioni, ambapo timu zote zilionesha ushindani mkali lakini zikashindwa kupata bao ndani ya muda wa kawaida.UTURO YAIBUKA KIDEDEA KWA MIKWAJU YA PENALTIBaada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo ya Uturo 0–0 Mtamba FC, hatima ya mchezo iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kwa upande wa Uturo, wapigaji waliofanikiwa kufunga ni Jadu Mpande, Hebron Msyani, Bura Mchape, Kwasi Jestoni na Rampadi Jafar. Ezeckia Wakundumbi na Mody walikosa penalti zao.
Kwa upande wa Mtamba FC, Gwakisa, Luko, Abraham na Sifa walifanikiwa kufunga, huku Waitoni, Hal and na Yona wakikosa mikwaju yao.Matokeo hayo yaliipa Uturo ushindi wa penalti 5–4, na kuibua furaha kwa wachezaji na mashabiki wa timu hiyo. Mchezo huo ulisimamiwa na mwamuzi Isaya Nakoli.
SOKA KWA AJILI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Rufiji Basin Cup 2026 ni sehemu ya shughuli za Mradi wa NBS Usangu, unaohamasisha jamii kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji, uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nishati safi na kupinga ukatili wa kijinsia.
Kupitia mashindano haya, soka linakuwa jukwaa la kuimarisha mshikamano wa jamii na kuifikisha kwa wananchi elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi rasilimali za asili.
Rufiji Basin Cup 2026 — Tunza vyanzo vya maji, linda mazingira, chagua nishati safi na pinga ukatili wa kijinsia!






































0 comments:
Post a Comment