Katika harakati za muziki zinazogusa mioyo, kuna nyakati ambazo msanii huamua kutazama nyuma — si kwa kujuta, bali kwa kusherehekea safari yake. Mei 16, msanii mahiri Zax 4Real atafanya hivyo kwa namna ya kipekee kupitia tukio maalumu linaloitwa "The Best of Zax 4Real", litakalofanyika katika eneo la kifahari la Pollo's Rooftop.
TUKIO HILI LITAKUWA LA AINA YAKE — PARTY YA KIMYA KIMYA - Silent Party — ambapo
kila mshiriki atasikiliza playlist maalum iliyoandaliwa na Zax 4Real, ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo zilizomjenga, kumtambulisha, na kumpa nafasi kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.NI SIKU YA MUZIKI, kumbukumbu, na hisia. Siku ya kuungana kama mashabiki, marafiki na familia ya ZAX 4REAL, tukikumbuka kila hatua aliyopitia na kusherehekea kwa nyimbo alizozitoa kwa upendo na maono. NI SIKU YA KUISHI TENA - kila wimbo kwa namna yako — kwa namna ulimfahamu Zax 4Real.
KIINGILIO
NI BURE KWA WAALIKWA WOTE, na kutakuwepo na mauzo ya vinywaji maalum vya
cocktails na mocktails kwa bei ya kirafiki ya 10,000 TZS tu. Hii ni nafasi ya
kukutana na mashabiki wengine, kufurahia burudani ya hali ya juu, na kuona Zax
4Real kwa jicho la karibu zaidi.
Zax 4Real anaahidi kitu kimoja: HAKUNA ATAKAYEBOREKA.
HII
NI ZAIDI YA PARTY — ni safari ya moyo kupitia muziki.
Kwa mawasiliano na maelezo zaidi,
tembelea instagram page ya ZAX 4REAL au jiunge na group maalumu la tukio hili.
MEI
16 — TUWE PAMOJA, tusikie, tukumbuke, tusherehekee.
0 comments:
Post a Comment