Kwa kuwa sasa umeanza kufanya kazi na msanii wako mpya), kuna mambo mengi ambayo utahitaji kurekebisha, kubadilisha na baadhi kuyaondoa ili uweze kuandaa na kutayarisha tangu mwanzo.
MJUE MSANII WAKO BORA
Jambo la kwanza unatakiwa kulifanya ni kwa namna tofauti kujua uwezo wa msanii na kufahamu kipawa chake. Kuelewa ubora wa msanii na udhaifu wake, na kufanyia kazi kwa sehemu ambazo zinapungukiwa. Vitu vya vinavyotakiwa kukaguliwa:-
Sauti yake/Vocal
Nyimbo zake/utunzi wake
Uzalishaji wa kazi zake
Uwasilishaji jukwaani
Uburudishaji
Muonekano
Uhusiano na vyombo vya habari
Chapa/brand
Mitandaoni
KUSHIRIKI KALENDA
Jambo la kwanza, msimamizi, utakuwa unasimamia kalenda ya msanii hivyo unahitaji kuisimamia na kuwa na accesss na kalenda ya wasanii na kuhakikisha kila mtu kwenye timu anashirikishwa kalenda hiyo.
VITU VYA KUKUSANYA/KUTENGENEZA/REKEBISHA
Mitandao ya kijamii, rekebisha maelezo yanayohitajika ikibidi
Wasifu wa Msanii, rekebisha ikibidi
Picha mpya, Kitabu kipya cha picha kinahitajika
Tuzo alizoteuliwa na kushinda, Hakikisha unazirekebisha na kuziweka ziendane na wakati na kuzihifadhi katika nyaraka moja.
Video za moja kwa moja, hifadhi link za video mahali pazuri
MAHITAJI MAALUM
Tengeneza na hifadhi jalada la Utumishi kwa timu ya tasnia(Meneja,Wakala),Watangazaji, Redio, Bidhaa, Mwanasheria, Mhasibu, Bima)
Simu ya moja kwa moja
Nambari ya simu ya ofisini
Barua pepe
Anwani
VITU VYA KUFANYA
- Sajili nyimbo
- Jisajili kwa uanachama ikiwa bado hujajiandikisha kwenye chama chako cha wanamuziki au wakala wako wa kukusanya nyimbo,majukwaa ya matamasha,mawakala wa matamasha n.k
Imeandikwa na Kizz1
0 comments:
Post a Comment