KUWA NA MALENGO
Hakikisha unakuwa na malengo ambayo unataka msanii wako ayafikie kwa kuzingatia vipaumbelehatua kwa hatua kwasababu kila msanii wako anapopiga hatua ni muhimu kujua nini kinafuata.
KUWA NA MPANGO
Ni vyema na lazima uwe na mpango (Plan) wa nini unatakiwa kufanya ili kufanikisha malengo ya msanii wako huku ukizingatia kuwa msanii pia nay eye ana mipango yake ambayo angependa kufanikisha. Hivyo ni muhimu katika ufanyaji kazi wenu mipango yenu iwe na uwiano ili muweze kufanikisha ufikiwaji wa malengo
TAMBUA MAJUKUMU YAKO
Hii itasaidia kila mmoja kuwa kiongozi kwenye nafasi yake na kwa kiwango stahiki katika kufanikisha malengo husika.
KUWA MVUMILIVU
Kuna wakati msanii atakuangusha au wewe utamuangusha msanii wako,kuna wakati msanii atafanya tofauti na mipango na maelekezo,usichoke wala kukata tama,kuwa jasiri na mvumilivu wa kuhakikisha hamtoki nje ya malengo mliyojiwekea.
JENGA UAMINIFU
Vitu vingi vya msanii kikazi na wakati mwingine binafsi utakuwa unahusika navyo moja kwa moja na vingine ni nyeti sana hivyo unatakiwa kuwa mwaminifu sana kwake na msiri pia. Uaminifu huo utakufikisha mbali sana wewe pamoja na msanii wako.
MWISHO
Kuna wakati utapokea pongezi na kuna wakati utapokea lawama kwa kazi unayoifanya,jifunze kujitathmini wewe mwenye kabla haujatathiminiwa kwa kila hatua unayopiga wewe na msanii wako maana mameneja wengi wanafanya kazi nyuma ya pazia. Mameneja wengi wanafanya kazi zao nyuama ya pazia na kazi za msanii zikiwa zinaenda vizuri huwa hawaonekani ila kukiwa na tatizo hapo ndio lawama zinaanza kuangukia kwa meneja na kuanza kumtafuta na kumuangushia zigo la lawama. Thamini namna mbalimbali zinazoleta tija kwenye kazi yako.
Imeandalia na kuandikwa na Kizz1
0 comments:
Post a Comment