Wednesday 8 May 2013

DIRECTOR MAARUFU WA FILAMU ASHIKILIWA NA POLISI KWA UTAPELI

 
Director na msanii maarufu jijini Mbeya Leonard Beleji maarufu kwa jina la JONLEE anashikiliwa na jeshi la polisi kituo kikuu jijini Mbeya kwa tuhuma za kumtapeli msanii wa filamu wa kike wa jijini hapa anayeitwa BEATRICE maarufu kama TRICE (anaeonekana kwenye picha).
Akizungumza na blog hii Trice anasema walianza kushoot Filamu hii tangu mwezi wa sita mwaka jana na baada ya kumaliza kushoot alichukua 'demo' kwa ajili ya kwenda kutafuta wadhamini na wasambazaji Dar baada ya kuzunguka sana hatimaye akapata wadhamini na wasambazaji waliohitaji MASTER ILI wasaini mkataba.
 
TRICE anaongeza kuwa baada ya kuanza kudai hiyo master hapo ndio kalenda na kukwepana kulipoanza baada ya kumffuatilia kwa muda mrefu ndipo akaamua kutafuta ushauri na kwa watu wengine ili wamsaidie kupata haki yake.
Akiwa kwenye mchakato wa kuhakikisha anapata haki yake bila kufikishana kwenye vyombo vya sheria ndipo tetesi ziliposambaa kuwa filamu ile ipo tayari dar es salaam na hajui imefikaje ndipo Trice alipoamua kuamua kuihusisha Polisi katika sakata hili ili haki ipatikane.
TUNAENDELEA KUFUATILIA SAKATA HILI mpaka tuone mwisho wake...stay tuned.

0 comments:

Post a Comment