Wednesday, 24 April 2019

SELEMENTALY NA FACT ZA U-KING (UFALME) WAKE MBEYA

Kumekuwa na wingu kubwa juu ya ufalme aliojitangazia mwana HipHop SELEMENTALY kwamba yeye ndiye mfalme wa muziki Mbeya na Kupitia media mbalimbali Selementaly amekuwa akifafanua juu ya ufalme wake. Anasema bila kuwakosea heshima watangulizi wake kwenye muziki,ukimuondoa SUGU yeye ndiye mfalme kamili wa Mbeya kwa kuzingatia fact zifuatazo hapa chini.

Hizi hapa ndio FACT za ufalme wake:-

1) ALBAMU MBILI za ukweli - mimi ndiye msanii pekee Mbeya niliyeproduce albamu mbili kwa mtaji wangu mwenyewe na kuziuza kila kona ya nyanda za juu kusini na rekodi yake kuwa wazi.
 - Albamu ya kwanza niliuza nakala 4,200 rekodi zipo
 - Albamu ya pili niliuza nakala 3,500 rekodi zipo
MCB

Kwa kuzingatia maelezo yake burudanimbeya tuliamua kufuatilia kwa wasanii wengine waliokwishato Albamu zao lkn hatukupata rekodi zinazoeleweka ingawa kwa idadi ya wingi wa albamu anazidiwa na Zax for real.

2) YOUTUBE CHANEL SUBSCRIBERS NA VIEWS - Nina subsribers zaidi ya 1650 kwenye chanel yangu na nina video yenye viewer zaidi ya 35,000 (35k).

 Sele na Bele9

Kwa kuzingatia maelezo yake burudanimbeya tuliamua kufuatilia kwa wasanii wengine tukagundua wasanii wengi hawafikishi hata subscriber 100 na wachache sana wana 100+ huku views wengi hawafikishi hata views 500 na wachache wana 2000+

3) VIDEO KALI - Nina video kali zaidi ya saba zenye viwango vya kuchezwa kwenye media house yoyote duniani.
Kwa kuzingatia maelezo yake burudanimbeya tuliamua kufuatilia kwa wasanii wengine na kugundua kuwa wasanii wengi hawana video kabisa au wana video ambazo hata wenyewe hawewezi kuziangalia kwa sababu ni mbaya na wenye video nzuri labda video moja.

Kwa kuzingatia fact hizo sisi kama burudanimbeya tunampongeza SELEMENTALY na kumtakia mafanikio zaidi kwenye safari yake ya muziki.

kwa maoni/ushauri/maswali au taarifa wasiliana na sisi kupitia burudanimbeya@gmail.com



0 comments:

Post a Comment