Tuesday 6 December 2016

HEKAYA ZA STIMELA - UHURU USIO HURU WA AMINA CHIBABA


Ukitazama harakati za akina J K Nyerere, patrice Lumumba, Samora Machel, Madiba tata Nelson Mandela na wengine wengi waliopambana kupata uhuru wa bendela wa nchi zao sio siri utagundua neno UHURU ni pana kuliko watu walivyolielewa,
Usifanye masihara na kutaka kuwa huru lazima upambane kweli kweli uvuje jasho na damu, upoteze mali na jina ili baadae uvijenge tena, kuwa huru sio kitu cha mchezo mchezo,
Nasema uhuru ni mpana maana unaweza jiona huru upande mmoja na upande mwingine haupo huru kabisa, ama unaweza kujiona upo huru lakini jamii inayokuzunguka inakuona umefungwa na minyororo kila kona inayokufanya ushindwe kupiga hatua moja mbele kama hujitambui utakaa hapo mpk utazeeka utasingizia umelogwa,
Dhana nzima ya watu kujitambua na kujitathmini iwapo wapo huru ama ni makoloni imekuwa ngumu sana sio tu kwa wasanii bali hata wananchi wa kawaida,
Lazima tujiulize yafuatayo;

1. Nina uhuru wa kuyasikiliza mawazo ya nafsi yangu?
2. Nina uhuru wa kusikilizwa mawazo yangu na watu wengine?
3. Nina uhuru wa kusikiliza mawazo ya watu wengine?
4. Nina uhuru juu ya kipato changu kuanzia kukitengeneza mpk kukitumia?
5. Nina uhuru wa kusimamia ninachokiamini bila kuyumbishwa kwa namna yeyote?
6. Nina uhuru wa kuwa huru?
7. Nina uhuru wa kuamua kutokua huru?
8. Nina uhuru wa kukubari au kutokubari au kukubari kutokubariana na jambo lolote?
9. .......Tunaruhusiwa kuongeza
Na mengine mengi tu aisee uhuru ni mpana sana usicheze na uhuru!!
Ni mapema sana mwishoni mwa mwezi wa october ama mwanzoni mwa december Nilimsikia msanii Amina Chibaba akihojiwa na DJ Frank wa Rock Fm katika udadisi wake wa kinini kilichotokea baina yake na T. Motion mi sijataka kujikita katika chanzo ila najikita katika sababu iliyotolewa na msanii husika kuwa "anaitaji kuwa huru" kwa maana harisi muda wote wa kuwa na T.motion hakuwa huru, alizingatia nini na kujiona ni koloni la T.motion anajua mwenyewe Ammychiba ila swala ni kuitaji uhuru, aina ya uhuru aliokuwa anautafuta hilo analijua mwenyewe Ammychiba,
Waswahili wanasema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Filauni, siku ya siku ikawadia wadau wakaa kuutafuta UHURU wa Ammychiba
Mambo yalikuwa mambo maana nilichosikia ni malalamiko ya Amina kutotimiziwa mahitaji yake!
Nikajiuliza UHURU ni kutimiziwa mahitaji?
Ni wazi ulikuwa wajibu wa T.motion kufanya hivo, nikagundua dada yangu kashindwa kutofautisha uhuru anaoutaka na wajibu anaopaswa kutimiziwa ni sawa na kushindwa kutofautisha TV na ITV kuwa ni vitu viwili tofauti,
Ni hadaa zilizoongozwa na dr. FAZ na pozi zake za kung'ata vidole zilitosha kugeuza mawazo ya Binti yule akageuza njia ya kanani na kurudi Misri,
Lile basi la zamani Fazi na Robart wamebadili matairi tu ila injini ileile
"Matairi tu yamefanya Amina alione jipya Tena"
#via uhuru wa kuongea nachowaza!!

0 comments:

Post a Comment