Tuesday, 10 May 2016

WASANII,WATANGAZAJI na WADAU WA MUZIKI MBEYA WAPEANA SOMO


Hii ilitokea kwenye kundi moja la Whatsapp linalounganisha wadau mbalimbali wa Muziki jijini Mbeya. Mjadala huu ulianza mara baada ya mtangazaji mkongwe na anayeheshimika sana Mbeya na watangazaji wenzie pamoja na wasanii ndugu Smart B kuandika maoni yake juu ya maendeleo ya muziki wa Mbeya. Yafuatayo ni majadiliano yalivyokuwa :-



Mbeya bhana kuna mambo ya ajabu sana,unajua kama mtangazaji na msanii au producer ni bora kujijua upo sehemu gani,umaarufu wa kijinga na sifa za kijinga mwisho wake ni umasikini,wewe mtangazaji jielewe au mtu yeyote aliye kwenye sanaa kuliko unafanya kazi nzuri unaipromote na pesa then show wafanya bure sawasawa na mtangazaji kuhost show bure hii inaua thamani ya kazi zetu ebu tubadilike ili kufikia malengo la sivyo utaishia umaarufu hata nyumba hujapanga,shit!?Team sio kwa ubaya,Team badilikeni.Thanx - Smart B
"NASIR" Fact smart bonge moja la point
"SMART" Yes broo hii sio kwa wasanii tu hata maisha ya watangazaji wenzangu nadhani mnayaona so kuwa wasamani na utaonekana wa samani yapo Dis ni zipo kila siku tusiogope kinachobidi ni kujitambua tu, ni aibu kubwa msanii kuwa na maisha mazuri kuliko mtangazaji na sisi tunategemeana.
"NOLESY" Na kitu kingine mkiupa nguvu muziki wa nyumbani maisha mazuri mtayaona ila ikiwa promo 'F' unaandaa show unategemea atakuja nani zaidi ya mashabiki zako.
"LUSEKELO" Kuna kitu kinaitwa mgawanyiko wa majukumu katika sanaa:-
1) Msanii ajitambue na atambue anafanya kazi sio starehe-tunga vizuri,tunza heshima kuanzia kwa producer,presenter&dj,promoter,manager,fans,fellow artits etc
2) Producer jua kuwa unafanya kazi ili upate wateja na ukuze ujuzi wako,heshimu ofisi sio nyimbo mbovu unarekodi,saidiana na artist kulink na media kusamabaza kazi
3) Presenter zipe nafasi ya kutosha kazi nzuri zinazofanywa na artists coz ukisapoti hizo kazi zitafanya wasanii wajulikane na hata ikifikia wakati unaandaa tamasha lazima mashabiki watakuja hicho kitasababisha mtangazaji uliyeandaa show na msanii wote mkaingiza kipato na maisha yakaenda vizuri
4) Fans wawe wanahudhuria matamasha sio kusufia kwenye mitandao tu au selfie na drFazi.
5) SARMY CLEVER Tukiungana tutatusua wote na hela tutapiga
6) NASIR GREEN Ubora wa studio ni tatizo,mbeya kuna studio zaidi ya 100 lakini zenye ubora hazizidi hata 10
7) LUSEKELO Tunahitaji workshop moja kubwa sana itakayounganisha wadau wote wa sanaa
8) Kitu kingine kinakuja pale ambapo managers wa radio hawatengenezi mazingira rafiki ya redio na wasikilizaji.

0 comments:

Post a Comment