Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, msanii chipukizi Zuuh Winner ameandika historia ya kipekee katika muziki wa Tanzania. Bila kuwa chini ya lebo yoyote au kundi lolote la muziki, na kwa msaada wa mashabiki, media zenye moyo, na meneja wake anayejulikana kwa jina la “Unga Unga”, Zuuh ameweza kuvuka mipaka na kutambulika kama Malkia wa Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Songwe, Sumbawanga, na maeneo mengine mengi ya Nyanda za Juu Kusini.
Katika muda huo mfupi, Zuuh ameweza kuvutia zaidi ya wafuasi 11,000 kwenye Instagram, zaidi ya 1,000 kwenye YouTube, huku akipata maelfu ya views kutoka ndani na nje ya nchi. Hii si mafanikio ya kawaida kwa msanii anayejiendesha bila msaada wa taasisi kubwa. Ni matokeo ya kazi ya bidii, kipaji halisi, na msaada wa mashabiki waliomwamini tangu siku ya kwanza.
“Hakuna mimi bila wewe shabiki yangu. Usiache kunishika mkono,” alisema Zuuh kwa hisia kali, akionyesha namna ambavyo mashabiki wake ni msingi wa mafanikio yake.
Zuuh pia ametumia nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa waandishi wa habari, watangazaji, DJs, na producers wa Tanzania waliompa nafasi bila kumtaka rushwa ya fedha wala ya ngono. Katika mazingira ambapo changamoto hizi ni za kawaida kwa wasanii wapya, ushuhuda wa Zuuh ni wa kipekee na unahamasisha wasanii wengine kuamini kuwa mafanikio yanawezekana kwa njia ya haki na maadili.
Katika hotuba yake, Zuuh alisisitiza kuwa ataendelea kushikilia
misingi hiyo ya ukweli, heshima, na kujituma:
“Mimi binti yenu, Zuuh Winner, naapa kwa maandishi haya sitawaangusha.”
Mashabiki, vyombo vya habari, na wadau wa muziki wameendelea kuonyesha
mapenzi ya dhati kwa msanii huyu mchanga ambaye sasa anatambulika kama “Queen
of Southern Highland” — jina alilopewa kutokana na ushawishi wake mkubwa
katika maeneo hayo.
Kwa sasa, Zuuh anaendelea kurekodi kazi mpya, kushiriki matamasha mbalimbali, na kukuza brand yake kwa kushirikiana na vituo kama: @mufindifm, @sdpupdates_mbeya, @dreamfmtz, @jembefmtz, @wasafitv, @mbeyacityfm, @crowntvtz,@burudanimbeya na wengine wengi waliomuamini kabla ya jina lake kuwa kubwa.
Kwa mawasiliano ya media, interviews au bookings: zuuhwinner@gmail.com
Instagram: @zuuh_winner
Tanzania – Southern Queen
0 comments:
Post a Comment