Kupitia playlist hii, @zax_4real2020 analeta pamoja nyimbo zake bora zilizowahi kutikisa anga la muziki wa Bongo Fleva, bila kujali mwaka au tarehe ya kutolewa kwake. Lengo ni kutoa heshima kwa kazi zilizojenga jina lake na kumpa nafasi ya kipekee katika historia ya muziki wa Tanzania.
“Muziki
mzuri haupitwi na wakati. Unastahili heshima, unastahili kusikika tena na
tena,” amesema @zax_4real2020.
“Naamini mashabiki wangu wanahitaji
kurudi kwenye kumbukumbu na kufurahia kazi ambazo ziliwahi kuwasisimua.”
Mbali na kutengeneza muziki wa kiwango cha juu, @zax_4real2020 ameendelea kuonesha ubunifu na uthubutu kwa kuandaa matamasha na maonesho makubwa, hususan katika Nyanda za Juu Kusini, ambako anatajwa kama msanii namba moja kutokana na ushawishi wake na mapokezi makubwa anayopewa na mashabiki.
Mashabiki na
wadau wa muziki wanahamasishwa kushiriki katika kusherehekea kazi hizi kwa
kusikiliza #Zax4RealBestPlaylist na kuendeleza mjadala wa ngoma bora zaidi
kutoka kwake. Aidha, mashabiki wanakaribishwa kushiriki kwenye kampeni ya
mitandaoni kwa kutaja show ya @zax_4real2020 ambayo huwezi kuisahau, au ngoma
yake ambayo kwako ni ya milele (timeless classic).
0 comments:
Post a Comment