Friday, 11 April 2025

FUNDISMART KULETA MAPINDUZI KWA MAFUNDI TANZANIA KUPITIA KONGAMANO LA MAFUNDI MBEYA 2025

Katika juhudi za kuinua mafundi wa Tanzania, FundiSmart kwa kushirikiana na LODHIA Industries pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeandaa tukio kubwa la kitaifa – Kongamano la Mafundi Mbeya 2025. Hili ni jukwaa mahususi kwa mafundi wa aina mbalimbali Kurasimisha, kujifunza, kushirikiana, na kujinufaisha kwa fursa mbalimbali za maendeleo ya kitaaluma na kiuchumi.

Mahali: Tughimbe Hall, Mafiat – Mbeya

Tarehe: Jumanne, 29 Aprili 2025

Muda: Kuanzia saa 2:00 asubuhi

Kiingilio: BURE kabisa!

MAFUNDI WANA NDOTO – FUNDISMART INAZITIMIZA

Katika kongamano hili, FundiSmart inalenga kuwakutanisha mafundi kutoka sekta mbalimbali kama vile:

-          Fundi umeme

-          Fundi kushona

-          Fundi uashi

-          Fundi bomba

-          Fundi magari

-          Fundi wa vifaa vya elektroniki

-          Fundi seremala, na wengine wengi

Kupitia jukwaa hili, mafundi watapata nafasi ya kipekee ya:

KUJITANGAZA KITAIFA

Kwa kujiunga na FundiSmart, mafundi wataweza kutangaza huduma zao na kuunganishwa moja kwa moja na wateja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa njia ya kidigitali.

KUPATA CHETI CHA VETA

Fundi yeyote anayefanya kazi ya ufundi bila kuwa na cheti rasmi, atapata nafasi ya kuthibitishwa kitaaluma kupitia cheti cha VETA. Hii ni hatua muhimu kwa mafundi wanaotafuta ajira, kandarasi za kazi au kushiriki zabuni za serikali na mashirika binafsi.

KUJIFUNZA MBINU ZA KISASA

Mafunzo maalum yataendeshwa kwa lengo la kuboresha ujuzi na maarifa ya mafundi ili waweze kushindana katika soko la kisasa la ajira na huduma.

KUPATA MIKOPO NA BIMA

Kwa kushirikiana na taasisi za kifedha, FundiSmart itawawezesha mafundi kupata mikopo ya vifaa vya kazi, mitaji midogo, pamoja na huduma za bima kwa ajili ya ulinzi wa maisha na kazi zao.

KUSHIRIKI MAKONGAMANO YA KITAIFA

Kwa kujiunga na FundiSmart, mafundi wanapata fursa ya kualikwa kushiriki makongamano kama haya yatakayokuwa yakifanyika katika mikoa mbalimbali, na hivyo kuwa sehemu ya mtandao mpana wa kitaifa wa mafundi.

JINSI YA KUJIUNGA NA FUNDISMART

Mchakato wa kujiunga ni rahisi na hauna gharama. Fungua simu yako kisha:
PIGA BURE *149*46*5# na fuata maelekezo.

Kwa mafundi wanaotaka kujijengea jina, kuaminika zaidi, na kufungua milango ya mafanikio, hii ndiyo nafasi yao adhimu.

Kongamano la Mafundi Mbeya 2025 siyo tu tukio la kawaida – ni harakati ya mageuzi. Ni wakati wa mafundi wa Tanzania kujifunza, kuthibitishwa, na kujiunga na dunia ya kidijitali na kitaaluma kwa usaidizi wa FundiSmart.

 

“FUNDI HUU NI WAKATI WAKO WA KUWA FUNDISMART.”


Usikose tukio hili. Njoo, jifunze, jiinue – kwa pamoja tujenge Tanzania ya viwanda kwa mikono ya mafundi mahiri!

0 comments:

Post a Comment