Monday, 14 April 2025

CATCHERMECHANICS ASHINDA TUZO YA BEST MUSIC PRODUCER KWENYE VWAWA FM AWARDS 2024

Katika tasnia ya muziki inayozidi kukua na kuimarika kila siku, jina la Catchermechanics limeendelea kung’ara kama moja ya majina makubwa yanayochochea ubunifu na ubora katika utengenezaji wa muziki. Mwaka huu, juhudi na kipaji chake zimethibitishwa rasmi baada ya kushinda tuzo ya Best Music Producer kwenye VWAWA FM AWARDS 2024.

Kupitia ujumbe wa shukrani alioutoa kwa mashabiki na wadau wa muziki, Catchermechanics alieleza furaha yake kwa heshima hiyo, huku akisisitiza kuwa ushindi huu haukuwa wa kwake peke yake, bali ni ushindi wa wote waliomwamini, kumpigia kura na kufuatilia kazi zake.

"Ahsante sana kwa wote mlionipigia kura na wote mnaonifuatilia. Kwa kweli nawaheshimu sana na ninathamini support yenu, nyinyi ndio mnaonipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii," alisema Catchermechanics.

Pia hakusita kuwapongeza na kuwashukuru washindani wenzake katika kipengele hicho, akiwataja @killer_soundstz na @stonee_mix, kwa kazi zao nzuri na ushindani wa heshima. Kwa Catchermechanics, ushindi huu ni motisha mpya ya kuendelea kutengeneza muziki wa kiwango cha juu na kuonyesha kuwa sekta ya muziki ina mashindano yenye afya na maelewano.

Aidha, alitoa pongezi kwa waandaaji wa tuzo hizo, @tuzo_za_vwawa_fm na @vwawa_fm, kwa mchango wao mkubwa wa kutambua na kuhamasisha vipaji vya wasanii na producers wa Tanzania, akiwataka kuendeleza utaratibu huo kwa miaka ijayo.

Katika salamu zake za mwisho, Catchermechanics hakusahau kumtaja mshirika wake wa karibu kwenye muziki @nala_mzalendo, ambaye pamoja walifanikiwa kuachia albums mbili kati ya tatu walizozitengeneza mwaka jana. Ushirikiano wao umeleta ladha mpya kwenye muziki wa Bongo na kuonesha kuwa mafanikio haya ni matokeo ya kazi ya pamoja na uaminifu wa kweli.

Kwa sasa, Catchermechanics ameahidi kuendelea kutoa kazi bora zaidi na kuendelea kushirikiana na vipaji vipya na vya zamani, kwa lengo la kupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

3 comments:

  1. Much love I appreciate it brother.....U Write Great Content

    ReplyDelete
  2. Nakubali One Love

    ReplyDelete
  3. General Catcher Mechanics Mtu Mbad

    ReplyDelete