Saturday, 28 October 2023

Chimo Grand ni Mbalamwezi Iliyotawala Anga

Ni saa 18:22 jioni tarehe 19 june 2021 kwenye V.I.P PARTY ya ZAX 4REAL with RAPHA INN HOTEL ndani ya viunga vya Hotel ya Rapha Inn kidogo utulivu unapotea kiasi baada ya kuingia watu wanne ambao baada ya kuingia tu kukatokea kidogo ubize wa kusalimiana na watu mbalimbali kitu kilichosababisha kukosekana utulivu kwenye event kwa muda lakini ghafla utulivu unarudishwa sauti iliyopangiliwa vizuri na kwa mpangilio wenye mvuto wa kipekee iliyokuwa ngeni kabisa kwenye masikio ya watu wengi kuanzia wale waliokuwepo mpaka wale walioingia muda sio mrefu (kumbuka hao watu wanne walioingia muda huo walikuwa ni wadau mashuhuri sana kwenye tasnia ya Sanaa ambao kwavyeo vyao wawili walikuwa ni mameneja wa redio,mmoja mkurugenzi wa chuo na mwingine alikuwa ni mkurugenzi wa management lebel ya wasanii).
Ule utulivu uliomteka kila mtu pale ulitoka kwa kijana ambaye kwangu mimi alikuwa ni mgeni kabisa kwenye masikio na macho yangu….basi wakati anaendelea kuimba nikaona wale manguli waliokuwa wameingia muda si mrefu wananong’ona jambo basi ikabidi nijisogeze karibu ili kusikia nini wanateta.
Mdau1: Oya mzee wewe si ndio baba wa wasanii wote inakuaje humjui huyu msanii sasa sisi ndo tutamjuaje? Sasa wewe baba gani?
Mdau2: Aisee hakiharibiki kitu hapa ngoja nifanye kitu
Basi mdau2 akamuita Zax na kumuuliza ‘Mwamba huyu dogo anayeimba umemtoa wapi?
Zax: huku akicheka ‘Boss mbona unafeli sana? Huyu dogo si unakumbuka nilishakupaga habari zake nikakuomba umsikilize na ngoma yake nilikutumia pamoja na namba yake ya simu ila naona hukusikiliza boss’.
Mdau2: Mwamba basi limeisha hili wewe nenda
Basi baada ya hapo nikaona mdau1 akamuta mtangazaji wa kwenye redio yake anayefanya kipindi cha burudani akimuagiza afanye live interview kwenye kipindi chake na siku atakayopanga kufanya naye interview amjulishe ili naye asikilize.
Baada ya hapo mimi nikarudi chap kwenye nafasi yangu ili wasijegundua kuwa nilikuwa nafuatilia mazungumzo yao. Nilipotulia kwenye siti yangu fasta nikafanya kufollow insta page ya yule mtangazaji pamoja na redio halafu nikaturn on notification.
Hayawi hayawi mara nikaona post kwenye insta page kwamba siku hiyo kuna interview ya huyo msanii kwenye kipindi cha redio basin a mimi nikaweka ratiba vizuri ili zisiingiliane na muda wa kusikiliza interview.
Nilianza na kipindi kuanzia kinavyoanza mpaka ikafika muda wa interview kama kawaida mtangazaji akaanza na kutengeneza mvuto kwa utangulizi mzuri kitu kilichozidi kuongeza hamu ya kusikiliza.
Mtangazaji alianza kwa kumkaribisha msanii na kumuachia nafasi yeye msanii ajitambulishe vizuri maana yeye mtangazaji alikuwa hana taarifa za kutosha za msanii.
Mtangazaji: Karibu sana kwenye kipindi jisikie huru kabisa,leo mimi na wewe ni mara ya pili tunaonana,mara ya kwanza tulionana kwenye event halafu leo ni mara ya pili,naomba tumia nafasi hii kujitambulisha kwa ufupi sana ili msikilizaji aweze kukujua.
Msanii: Asante sana ndugu mtangazaji,jina langu kamili naitwa MUSSA SAMLI MMACHIMO na jina la kazi yangu ya Sanaa najulikana kwa jina la CHIMO GRAND ambalo nimechukua kwa kukata mwishoni mwa jina langu la mwisho.
Jina langu "chimo grand" nilianza kulitumia 2018 mwishoni  nikiwa Advance School katika shule ya Ivumwe sec school,  na kabla ya hapo nilikuwa nikijulikana kama DECENT PERSON ambalo nilipewa na rafiki zangu kipindi nipo o'level shule ya sekondari WENDA.  
Mtangazaji: Lini uligundua kuwa unajua kuimba?
Chimo: Kipaji changu cha muziki kilianza kutambuliwa na mwalimu wangu wa shule ya msingi alikua akiitwa Mwl.John ambaye alikua akiniona naimba peke yangu na kuamua kuniimbisha mbele ya darasa na ndio ilikua mara yangu ya kwanza kuimba mbele za watu kisha nlikabidhiwa sh.2000 mbele ya darasa mwaka 2012. 
Mtangazaji: Nini kilifuata baada ya hapo?
Chimo: Baadaye nikawa naendelea kuimba hata nlipoingia secondary na baadae nikaja kufanikiwa kukutana na rafiki aliyenizidi kidogo umri ambaye tulisoma pamoja tuition alitambulika kama GADO Mc ambaye alipenda ninavyoimba na kunitambulisha kwa rafiki yake mwengine aliyeitwa KELV Mc (Producer aliyetengeneza wimbo wa Green Boy – Chuchumaa,wimbo wa Zax & IQ – Rafiki Adui na wimbo wa Meshamazing – Sina Thamani) ambaye pia alinitambulisha kwa rafiki yake mwengine ambaye alikua ni producer aliyefahamika kama LIL France. Producer huyo aliyenikaribisha ofisin alipokua anafanyia kazi pale South Side music. Hapo ndo ikawa mara yangu ya kwanz kuingia studio japo sikufanikiwa kufanya kazi,lakin nlifahamiana na kaka mpya kwangu aliyejulikana kama zax 4real ambaye alikuja kuwa daraja langu kwa baadhi ya maeneo,alinishauri na kunipa elimu nyingi sana kuhusu muziki.
Mtangazaji:Umesema pamoja na kufika South Side Music lakini hukufanikiwa kurekodi,je jitihada au hatua gani ulizifanya mpaka leo tunazungumza na wewe?
Chimo: Nlikuwa mtu wa kupammbania tu kupata nafasi na kwenda studio mbali mbali kufanya mazoez hasa studio ya Z inc rec iliyokuwa chini ya producer Majeshi na kwa bahat nzuri nkapata lebel kwa mara ya kwanza  katika studio za ONETIME rec zlizokua chini ya Bix nyota, na huko ndo nilianza kufanya kazi na kurecord, baadae nikahamia Power records iliyokua ikisimamiwa na producer CUDO B na baadae nikaenda Jamvibes iliyokuwa chini ya  Bob Lau mmiliki wa Kiwira motel Soweto ndipo nilifanikiwa kutoa wimbo wangu wa kwanza ulionipeleka radio kadhaa za mbeya japo haukua na mafanikio ila ulinifanya nipate kufahamika zaidi mazingira ya chuo kwa kuwa nilikuwa mwanachuo na nilishiriki mashindano mbalimbal nikashinda. 
Baadaye nikajiunga na kundi la wanachuo wenzangu tuliloliita C.H.T kwa maana ya CUCOM HOUSE OF TALENT nilijifunza vitu vingi sana nikiwa katika kundi kama mwenyekiti wa kundi hili lililokuwa na wasanii kama Smile kiss, mzimba, last king, punchline dr, na shark.
Baadae kundi lilivunjika na kujitafuta kila mtu na njia yake, hapo ndo nilipoamua kumtafuta Mtangazaji MR TEE Kilaka Mashine na kumuomba anisimamie lakini kwa ubize wa kazi akaniambia mdogo wangu nitakutafutia mtu na baadae alinitafutia mtu aliyeitwa KING FAJA BAMS tukafanikiwa kuachia nyimbo iliyonipa mafanikio mengi sana ikiwemo show nyingi za kulipwa, mashabiki wengi na pia ilifanya nipate nafasi ya kushiriki mashindano ya BSS ALLSTARS  ambayo tulikwenda wawakilishi watatu kutoka mbeya na kwa bahati nikaweza kuiwakilisha mbeya mpaka hatua ya top 20. Mpaka sasa nafanyakazi KING FAJA BAMS tukiwa na ushirikiano wa karibu sana na producer Deo touchez.
Mtangazaji: Maswali yangu mimi yameishia hapa ila nataka nikwambie kitu mdogo wangu,HONGERA sana unajua sana kuimba na huwezi amini hii interview tunayofanya na wewe hapa ni boss alinipa maagizo nifanye interview na wewe na ameisikiliza yote tangu tunaanza mpaka muda huu halafu kuna ujumbe wako kanitumia hapa nitausoma mwishoni kabisa wakati tunamaliza
Chimo: Asante sana,sina cha kuongea Zaidi ila nitaendelea kupambana ili Imani mliyonipa isiende bure
Mtangazaji: Meseji ya boss inasema ‘Pekua wasanii wote wanaoimba,pekenyua nyimbo zote za wanaoimba ziweke kwenye mzani wa Chimo zote zitaelea,sio kwamba nasema hivyo kwa ajili ya kuwakosea heshima wasnii wengine ila ni kwa kile alichokionesha siku ile kwenye event lakini pia alichokionesha leo hapo studio’ yaani akiimba akapela perfect tumesikia hiyo aliyorekodi balaa so huyo msanii ni madini yenye thamani kubwa sana duniani ila sema tu hayajashtukiwa. Lakini pia kwa muonekano na kujieleza yupo very class na heshima sana.
Basi baada ya kumaliza kusikiliza interview kuna sauti kutoka ndani ikawa inaninong’oneza ikisema ‘kushuhudia ukubwa wa kipaji hiki na kukaa kimya bila kusema na kusapoti wakati nafasi unayo ni dhambi kubwa’. Namalizia kwa kusema Chimo grand ni mbalamwezi iliyotawala anga.
Baadhi ya nyimbo zake zinazotamba ni;-
CHECHE
BADO 
RAHA

1 comments: