Friday, 27 October 2023

Ambulance Amos ni UBAO WA KUSOMEA AHESHIMIWE

Kutoka kwenye unabii mpaka kuwa mchizi wa Gheto,Yes Ambulance Amos au muite LITAMA Boy mjukuu wa Skeleton mwamba imara wa Nzovwe nguzo ya Mbeya.
Upepo mkali sana ulioambatana na vumbi unavuma kutokea upande wa Halengo unanikumba hapa kwenye kichochoro cha kuelekea uwanja wa Shule ya msingi Nzovwe nyuma ya nyumba ya Balozi mama Silungu huku nikiwa nimefumba macho yangu kuzuia vumbi lisiingie machoni kwa mbali upande wa pili nasikia wimbo wenye baadhi ya maneno kama ‘siku zinakwenda (niokoeni)’…..Yes ni wimbo wa WAWASKE – Prophet Amos x Jenerali Adam unaoitwa NIOKOENI mara upepo unakata nafumbua macho yangu naona mbele ya macho yangu ilipokuwa Camp ya WAWASKE ndipo kumbukumbu zangu zinaporudi mpaka kuazia miaka ya 2006 na namkumbuka Zaidi Ambulance na baadhi ya matukio yake muhimu kwenye muziki.
Alianza muziki wake akijulikana kwa jina la Prophet Amos kupitia kundi lake lililojulikana kama WAWASKE (Wajukuu Wa Skeleton) akiwa na Swaiba wake Adam a.k.a Jenerali likiwa na makazi yake Nzovwe pembezoni mwa shule ya msingi Nzovwe Mkoani Mbeya walitamba sana na wimbo wao ulioitwa NIOKOENI waliourekodi chini ya marehemu Complex.
Ambulance Amos ni msanii aliyetoka katika generation ya kina Izzo B,Tox Star,Watukufu Camp n.k na ameshafanya event nyingi sana kubwa kutoka kwa waandaji wakubwa,alizoandaa mwenyewe na kampeni mbalimbali kama baadhi zinavyoonekana hapa;-
EVENT SHOWS
- fiesta clouds fm 2008 - Mbeya
- likizo time magic fm 2010 - Dar
- Singida motel chrismas event 2012 - Singida
- mlimba town - Morogoro
- Miaka kumi ya made - Manzese
Ambulance amechukua tuzo kadhaa kama inavyoonekana hapa;-
TUZO 
Mkali wa rymes Mbeya 2008 iliyoandaliwa na Mbeya fm

MAFUNZO 
Music - bagamoyo tasuba - Vocal
Baadhi ya nyimbo zilizompatia umaarufu;-
- Niokoeni ft bakora
- wakati ndiyo huu ft Z anto
- Mapepe kinoma ft nay wa mitego
- ukienda nyumban ft tunda man
- Nasema basi ft water chilambo
Ambulance ameshawahi kuwa member wa tip top connection chini ya uongozi wa babu tale pamoja Abdul Bonge akiwa na wasanii wenzake kama Madee, z anto , pingu na deso, Tunda man, Jabari, Pnc, Mb dog na wengine.Pia ameshawahi kufanyakazi rock fm radio as presenter kwa miez 6 tu . Ambulance aliamua kusimama kufanya muziki kwa miaka saba huku akifanya mambo mengine yasiyohusiana na muziki mpaka alipoamua kurudi tena mwaka 2020 na kufanya show yake ya kwanza aliyojiandalia yeye mwenyewe iliyofanyikia pale katika ukumbi wa Tumanyene uliopo Nzovwe Mbeya iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa na kupelekea kumpatia nafasi ya kufanya kampeni za siasa na Dr.Tulia Ackson katika kata zote za Mbeya jiji.
Kwa sasa Ambulance anatamba na nyimbo kama;-
Bonge la Demu ft Mbantu
Usinibabaishe
Hapa ni wapi
Lazima uhonge ft Nay wa Mitego
Mwagilia moyo n.k
Alikuwepo kwenye mapinduzi ya muziki,akapumzika wakati muziki unakua amerudi wakati muziki tayari umekua na anakimbiza itoshe kumuita UBAO WA KUJIFUNZIA ambao kila mwanafunzi lazima auheshimu.

0 comments:

Post a Comment