Friday, 27 October 2023

ZAX 4REAL NDIYE ALAMA YA MUZIKI MBEYA ‘Apewe maua yake’

ZAX 4REAL NDIYE ALAMA YA MUZIKI MBEYA ‘Apewe maua yake’
ZAX4REAL NI NANI?
Zackaria Mwakalibule anayefahamika zaidi kwa jina lake la kisanii la ZAX FOR REAL anayeimba hasa muziki wa R&B pia Afro Pop na Bongo Fleva. Pia anafahamika kama RnB Soilder,Taifa,Mwamba,King Dingii n.k. 
SAFARI YAKE YA MUZIKI IMEANZIA WAPI?
Zax For Real alianza kuvuma mwaka 2014 baada ya kutoa kibao cha "SHE IS GONE" ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava. Baadaye akaja kutamba zaidi na kibao kama vile PUNGUZA HASIRA, PRISONER, NGOLELA, I AM A NEW ONE, Moyo Mashine, na nyingine kibao. 
Zax4Real ndiye msanii anayemiliki tuzo nyingi kuliko msanii yoyote Mbeya na nyanda za juu kusini,anakadiriwa kumiliki tuzo rasmi Zaidi ya kumi (10) na zingine zaidi ya saba ambazo hakuna msanii yoyote ukanda huu amefikisha hata nusu ya hizo tuzo.

Baadhi ya Tuzo rasmi anazozimiliki ni kama zinavyoonekana hapa
Year 
Nominee / work 
Award 
Result 

2016 
T-MOTION ENTERTAINMENT 
BEST MALE ARTIST 
Won 

2016
SUPER NYOTA
SUPER NYOTA
1st runup

2018 
BIG STAR FM 
BEST ARTIST OF THE YEAR
Won 

2019 
MBEYA FINEST AWARDS 
BEST MALE ARTIST
Won 

2020 
MBEYA FINEST AWARDS
BEST SINGER 
Won 

Lakini pia Zax4Real ndiye msanii anayeongoza kwa kufanya show nyingi ambazo ni zile alizoziandaa mwenyewe na zilizoandaliwa na wengine kama baadhi zinavyoonekana hapa
SHOWS KUBWA ALIZOPERFORM
MTIKISIKO (By Ebony fm) 2015
FEMA 2015
FIESTA (By Clouds Media Group) 2016
KUMEKUCHA DAY (By Bomba Fm) 2017
SHOWS KUBWA ALIZOZIANDAA MWENYEWE
PUNGUZA HASIRA 
MASK PARTY 
PRISONER
WHATSAPP FRIENDS PARTY 
I AM A NEW ONE ALBUM LAUNCH
RnB NIGHT 
UFALMENI DAY 
MTOTO WA MBEYA EVENT
N.k
Kingine cha ziada Zax ni msanii anayeongoza kuwashika mkono wasanii wanaochipukia,nani asiyejua namna alivyowashika wasanii wengi wanaochipuki kwa kuwaelekeza,kuwaonesha njia,kuwafundisha,kuwatia moyo,kushiriki kwenye nyimbo zao,kuwatambulisha kwa wadau n.k
Amepewe sifa na majina mengi sana yote ni katika kutaka kumpatia heshima yake,pamoja na yote hayo sisi tunasema itoshe tukimuita ALAMA YA MUZIKI WA MBEYA

0 comments:

Post a Comment