1. Muheshimu anayekununulia
2. Muamkie mtoa ofa kabla hujakaa kitini
3. Uwe ndie mchekeshaji wa kikao, lakini usimkatishe mazungumzo anaetoa ofaa
4. Daima jitolee kufuata na kubeba vinywaji toka kaunta
5. Mtoa ofa akikutuma popote usikatae
6. Mtoa ofa akiupenda muziki fulani, we anza kucheza kwa bidii kabisa
7. Usiwe msafi kuliko mtoa ofa
8. Usinywe kwa pupa, kunywa mafunda madogomadogo
9. Usitamani mpenzi wa mtoa ofa hata kama ndie mke wako
10. Mtoa ofa akitoa kichekesho cheka sana hata kama hakichekeshi KUMBUKA……Mtoa ofa akiwa Man U na wewe Man U, akiwa Chelsea na wewe hivyo hivyo. Akiwa CCM na wewe onyesha kadi kabisa, akiwa CHADEMA onyesha kadi na katiba…kifupi uwe umejitayarisha kila wakati.
Saturday, 11 May 2013
Amri kumi kwa wapenda ofa
Labels:
Vijana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment