Wednesday 4 September 2024

ORODHA YA VITU VYA KUZINGATIA/KUFANYA KWA MSANII WAKO UNAYEANZA KUMSIMAMIA

Kwa kuwa sasa umeanza kufanya kazi na msanii wako mpya), kuna mambo mengi ambayo utahitaji kurekebisha, kubadilisha na baadhi kuyaondoa ili uweze kuandaa na kutayarisha tangu mwanzo.

MJUE MSANII WAKO BORA
Jambo la kwanza unatakiwa kulifanya ni kwa namna tofauti kujua uwezo wa msanii na kufahamu kipawa chake. Kuelewa ubora wa msanii na udhaifu wake, na kufanyia kazi kwa sehemu ambazo zinapungukiwa. Vitu vya vinavyotakiwa kukaguliwa:-
Sauti yake/Vocal
Nyimbo zake/utunzi wake
Uzalishaji wa kazi zake
Uwasilishaji jukwaani
Uburudishaji
Muonekano
Uhusiano na vyombo vya habari
Chapa/brand
Mitandaoni

KUSHIRIKI KALENDA
Jambo la kwanza, msimamizi, utakuwa unasimamia kalenda ya msanii hivyo unahitaji kuisimamia na kuwa na accesss na kalenda ya wasanii na kuhakikisha kila mtu kwenye timu anashirikishwa kalenda hiyo.

VITU VYA KUKUSANYA/KUTENGENEZA/REKEBISHA
Mitandao ya kijamii, rekebisha  maelezo yanayohitajika ikibidi
Wasifu wa Msanii, rekebisha ikibidi
Picha mpya, Kitabu kipya cha picha kinahitajika
Tuzo alizoteuliwa na kushinda, Hakikisha unazirekebisha na kuziweka ziendane na wakati na kuzihifadhi katika nyaraka moja.
Video za moja kwa moja, hifadhi link za video mahali pazuri

MAHITAJI MAALUM
Tengeneza na hifadhi jalada la Utumishi kwa timu ya tasnia(Meneja,Wakala),Watangazaji, Redio, Bidhaa, Mwanasheria, Mhasibu, Bima)
Simu ya moja kwa moja
Nambari ya simu ya ofisini
Barua pepe
Anwani

VITU VYA KUFANYA
- Sajili nyimbo
- Jisajili kwa uanachama ikiwa bado hujajiandikisha kwenye  chama chako cha wanamuziki au wakala wako wa kukusanya nyimbo,majukwaa ya matamasha,mawakala wa matamasha n.k
Imeandikwa na Kizz1 

Tuesday 3 September 2024

NAMNA YA KUSIMAMIA MSANII

KUWA NA MALENGO
Hakikisha unakuwa na malengo ambayo unataka msanii wako ayafikie kwa kuzingatia vipaumbelehatua kwa hatua  kwasababu kila msanii wako anapopiga hatua ni muhimu kujua nini kinafuata.

KUWA NA MPANGO
Ni vyema na lazima uwe na mpango (Plan) wa nini unatakiwa kufanya ili kufanikisha malengo ya msanii wako huku ukizingatia kuwa msanii pia nay eye ana mipango yake ambayo angependa kufanikisha. Hivyo ni muhimu katika ufanyaji kazi wenu mipango yenu iwe na uwiano ili muweze kufanikisha ufikiwaji wa malengo

TAMBUA MAJUKUMU YAKO
Hii itasaidia kila mmoja kuwa kiongozi kwenye nafasi yake na kwa kiwango stahiki katika kufanikisha malengo husika.

KUWA MVUMILIVU
Kuna wakati msanii atakuangusha au wewe utamuangusha msanii wako,kuna wakati msanii atafanya tofauti na mipango na maelekezo,usichoke wala kukata tama,kuwa jasiri na mvumilivu wa kuhakikisha hamtoki nje ya malengo mliyojiwekea.
JENGA UAMINIFU
Vitu vingi vya msanii kikazi na wakati mwingine binafsi utakuwa unahusika navyo moja kwa moja na vingine ni nyeti sana hivyo unatakiwa kuwa mwaminifu sana kwake na msiri pia. Uaminifu huo utakufikisha mbali sana wewe pamoja na msanii wako.

MWISHO
Kuna wakati utapokea pongezi na kuna wakati utapokea lawama kwa kazi unayoifanya,jifunze kujitathmini wewe mwenye kabla haujatathiminiwa kwa kila hatua unayopiga wewe na msanii wako maana mameneja wengi wanafanya kazi nyuma ya pazia. Mameneja wengi wanafanya kazi zao nyuama ya pazia na kazi za msanii zikiwa zinaenda vizuri huwa hawaonekani ila kukiwa na tatizo hapo ndio lawama zinaanza kuangukia kwa meneja na kuanza kumtafuta na kumuangushia zigo la lawama. Thamini namna mbalimbali zinazoleta tija kwenye kazi yako.
Imeandalia na kuandikwa na Kizz1

Wednesday 7 August 2024

GREEN BOY MR ONE TOUCH

Miaka kadhaa nyuma kabla ya 2018 dhahabu hii iliishia kupotelea mchangani hakuna aliyejali wala Kujaribu kuitazama Kwa jicho la thamani mpaka pale majeshi ya Vibes kutoka T-Motion Entertainment yapotumwa kwenda kuichimbua dhahabu hii.
Haikuwa kazi rahisi kukubalika na kupata nafasi ndani ya taasisi kubwa ya T-Motion Entertainment pamoja na kwamba alikuwa ni mshirika wao wa karibu pia kuwa mshikaji wa karibu na msanii wao namba Moja kipindi hicho Meshamazing.
Energy, Vibes,creativity na spirit vinamfanya kuwa ndiye Best Male Artist wa Mbeya currently mpaka pale atakapokuja kupatikana mwingine maana tangu ametangazwa na kwenye tuzo za MBEYA FINEST AWARDS 2020 (anavyodai yeye mwenyewe)
Mabibi na Mabwana namleta kwenu Green Boy 'Wizard' msanii mkali wa kizazi kipya anayefanya mitindo aina zote ya muziki ambaye alianza kama msanii wa muziki wa utamaduni wa HIP HOP 
Swali: Ilikuwaje ukabadilika kutoka kuwa msanii wa muziki wa HIP HOP ambao tulizoea kukuona kwenye vilinge kibao vya HIP HOP mpaka Sasa unaonekana unafanya sana bongo fleva music?
Green Boy: kiukweli hii ilikuja kipindi nimepewa nafasi ya kuwasilisha ngoma Kwa uongozi Kwa ajili ya kuipeleka media nikawasilisha ngoma zaidi ya tatu nilizokuwa naziamini sana wakazipokea nakuzisifia lakini hawakufanya chochote basi kuna siku boss alipita studio akasikia kuna ngoma tulikuwa tunafanya pale studio na haikuwa kwenye mipango basi boss akamwambia producer malizia hiyo kazi nataka. 
Basi producer kesho yake akaimaliza akampatia boss then boss akaniambia nikapige picha Kwa ajili ya kutengeneza cover la wimbo na siku iliyofuata nikapewa ratiba ya interviews redio mbalimbali. Hivyo ndivyo wimbo wangu wa kwanza CHUCHUMAA uliokuwa na mahadhi 'danso hiphop' ulivyobadilisha kila kitu kwenye safari yangu ya muziki maana ulipokelewa vizuri sana na hadi ikapelekea kidogo Boss na father Lugombo kidogo kutupiana lawama maana Lugombo aliamini kwasababu boss ana wasanii wa pure bongo fleva basi kanilazimisha na mimi niende kwenye mlengo huo. Baada ya ChuchuMaa nikaja na Moja namba,Ngabhaghila ft Mwaisa Nyonyoma,ChapChap n.k
Swali: Wanakuita Mzee wa one touch yaani ukaingia tu Tmotion halafu Ngoma Moja tu ukaingia mainstream?
Green Boy: Si mchezo,iko hivi kaka,kabla ya kuingia Tmotion nimepita machimbi kibao na vilinge vingi sana...watu wengi wanadhani hivyo...mimi nimesota sana pale Tmotion sio chini ya miaka miwili ndio nikakubaliwa then baada ya hapo nikawasilisha ngoma nyingi kwa uongozi mpaka ikakubaliwa ChuchuMaa kuanza nayo lakini pia baada ya ChuchuMaa nilipigishwa featuring nyingi sana na wasanii wengine ili nipate uzoefu wa kutosha.
Green Boy ni mmoja ya wasanii walioteuliwabkwenye BIG20 Mbeya 
Itaendelea...
- Maisha yake pale Tmotion 
- Safari yake south Africa 
- Ushkaji wake na Meshamazing 
- n.k
Imeandikwa na kizz1

Tuesday 6 August 2024

NALA MZALENDO AACHIA ALBUM yake YA TANO

Mwanamuziki wa utamaduni wa HIP HOP kutoka jijini Mbeya SUDI ALLY MWAKILACHILE maarufu kwa jina NALA MZALENDO ameachia album yake ya tano yenye jumla ya nyimbo kumi na Moja (11) hivi karibuni akiipa jina la SON. NALA ni mmoja wa wateule 20 kutoka kwenye BIG 20 ARTISTS walioteuliwa na media personalities pamoja na wadau wengine wa Muziki kama sample kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya sanaa ya Muziki Mbeya akitokea MAKANTA AFRICA 
NALA mpaka Sasa anamiliki album 5,Ep 3 na Mixtape 1 zenye nyimbo zaidi ya 116 zilizopo kwenye Album,Ep's na Mixtape bila kuhesabu singles,collables na cyphers 
NALA ni mshindi wa tuzo ya msanii chipukizi Mbeya 2019
ALBUM NALA inapatikana kwenye digital platform zote pia unaweza kuipata Kwa kuinunua kwa 20,000/- Unatumiwa Kwa Email/Telegram/WhatsApp 
TIGO PESA 0719568535
(SUDI ALLY MWAKILACHILE)
Full story ya Maisha yake na Muziki itakujia soon kupitia jukwaa hii.

Imeandikwa na Kizz1

MBEYA YAJA NA BIG 20

Hii ni project/movement iliyoanzishwa na media personalities pamoja na wadau wa Muziki jijini Mbeya lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha kuwa Muziki na wanamuziki wa mkoa wa Mbeya wanapata jukwaa huru na la uhakika katika kufanya kazi zao. 
Wakiongea na jukwaa hili waratibu wa movement hii wanasema kuwa wameanza na wasanii hao 20 kama sample tu Kwa kuanzia lakini lengo lao ni kumfikia kila msanii wa Mbeya na ndio maana hata hao waliopendekezwa ni mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali waliopendekeza majina ya wasanii hao kwa kipindi cha wiki moja.
Wasanii walionza nao kwenye awamu hii ya kwanza ni:-
1 J - fish hunter
2 D - Garle
3 Miss geezy
4 Big Benk
5 Em one
6 Silvia Green
7 Young 40
8 Kali more
9 Smile kiss.                        
10 Zax B mtoto wa Boss
11 Samba melodie
12 Johym
13 Green boy wizard 
14 Nala mzalendo
15 Triple M dracula 
16 Selementaly 
17 Balone dope
18 Chimo
19 Dora boy (I-q de music)
20 Kwazee
Burudani Mbeya tunawatakia mafanikio mema katika movement hii 

Imeandikwa na Kizz1